Wanafunzi na walimu wa chuo kikuu cha ardhi wafariwa mafunzo juu ya urasmishaji wa makazi

Ujanibishaji wa sasa unafanyika ili kurasmisha makazi yasiyo rasmi ya Dar es Salaam ambayo sasa inafikia asilimia 70 ya jiji. Kurasimisha makazi kunasaidia kutoa uhalali kwa jamii na kuongeza usalama wa umiliki wa wakazi na haki zao za ardhi. Kujenga makazi pia kunaruhusu mipango zaidi ya kudumu ya mji. Kwa bahati mbaya, mbinu za sasa za ukusanyaji wa taarifa kuelewa mipaka hii imesababisha taarifa zisizo sahihi kutokana na ushiriki mdogo wa wanajamii. Ili kusaidia kuboresha mbinu za kukusanya taarifa za sasa zinazohitajika kwa ujanibishaji, timu ya HOT  Tanzania imetoa siku tatu za mafunzo…Read more

Hisia Za Kwanza/ Mwanzo Ramani Huria

Kwa sasa asilimia 70 ya miundombinu Dar es Salaam haijapangwa, maana yake ni kwamba miundo mara nyingi hujengwa katika maeneo ya mafuriko na haijatengenezwa kwa kutosha ili kukabiliana na maji mengi. Mara nyingi, hata majengo yasiyopangwa yaliyo ‘salama’ na mafuriko yana athari kubwa juu ya eneo jirani; Mpango usiofaa umesababisha ongezeko la udongo mgumu (Compact soil), ambao una viwango vya chini vya kunyonya maji ili kuzuia kusambaza maji wakati wa mafuriko. Ramani Huria ni mradi unaofanywa na HOT, kwa lengo la kuzalisha ramani kwa nia kuu ya kuboresha mipango ya ustawi wa mafuriko…Read more

Ramani za Mitaro kwa Ajili ya Kutengeneza Kielelezo Maalum cha Mafuriko

Ramani Huria 2.0 inakusanya taarifa za mitaro kwenye maeneo yaliyo katika hatari ya mafuriko Dar es Salaam. Taarifa hizi zinatumika kutengeneza programu/kielelezo maalum cha mafuriko (flood model) ambayo inahitaji taarifa za mitaro zilizokusanywa kwa usahihi kama urefu, upana, kama mtaro umeziba (kwa majani au vitu vingine), muunganiko na kipenyo (Kwenye kalavati).  Kutengeneza programu hii, Ramani Huria inafanya kazi na mtaalamu wa hydrolojia huko Deltares- Uholanzi, Hessel Winsemius. Dr. Hessel ni mtaalamu katika uwanja wa hydrolojia, hasa kwenye masuala ya kutengeneza vielelezo vya hatari ya mafuriko kikanda na kimataifa. Wiki hii alikuwa Dar es…Read more

Mkutano wa Hali ya Ramani Tanzania- 2017

Tarehe 8 hadi 10 Disemba Croud2Map na Ramani Huria walishirikiana kuandaa mkutano wa kwanza wa hali ya ramani uliofanyika Dar es Salaam, Tanzania. Mwanzoni tulitegemea washiriki 150 lakini watu waliofika walizidi makadirio yetu ya mwanzo na kufikia watu 170 kutoka nchi saba:  Malawi, Kenya, Uganda, Rwanda, Zambia, Ujerumani na Tanzania yenyewe. Ilikuwa tukio ambalo liliwaleta pamoja watu wenye taaluma tofauti tofauti kufanya mafunzo, kufahamiana na kushirikiana Washiriki; Mafanikio makubwa ya mkutano yalitokana na washiriki kuwa na taaluma tofauti tofauti. Waliohudhuria walikuwa watu kutoka Vyuo vikuu, Vijana watengeneza ramani, wanajamii, watafiti, viongozi wa serikali,…Read more

Ramani Kwa Ajili ya Siku ya VVU / UKIMWI Duniani- 2017

Katika heshima ya Siku ya UKIMWI Duniani 2017, Ramani Huria na Tanzania Data Lab (dLab) waliandaa tukio kuongeza ufumbuzi kwa njia ya uwazi, uwajibikaji na ushirikiano. Lengo ilikuwa watu kujifunza jinsi ramani inavoweza kuongeza uhuru na upatikanaji wa habari kwa umma juu ya VVU / UKIMWI katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania. Tuliamua kutengeneza ramani ya Geita wilaya iliyopo katika ukanda wa ziwa Victoria ambapo wilaya hii ni moja ya wilaya zinazongoza kwa ukatili wa kijinsia kutokana ukatili huu watu wamepata ulemavu wa moja kwa moja uliosababishwa na ukatili huo. Ni wazi kuwa maeneo…Read more

Kujenga Zana za Wazi kwa Ajili ya Kutengeneza Ramani za Mifereji

Lengo la Ramani Huria ni ustahimilifu: Kupunguza athari za mafuriko kwa binadamu. Njia ya kawaida kabisa ya kupunguza hili ni ni kuondoa uwezekano wa mafuriko! Mifereji ni moja ya njia ya kufanya hili. Culvert                                                          Concrete Drain Ditch                                                        …Read more

Uzinduzi wa Ramani Huria 2.0

Tarehe 26 Septemba 2017, ukurasa mpya wa RAmani Huria 2.0 ulifunguliwa rasmi kwenye ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Tukio lilihudhuriwa na wadau muhimu wakiwemo maafisa wa serikali, maafisa wa vyuo vikuu, Washiriki kutoka kikosi  cha msalaba mwekundu, wataalamu wa ramani, wana jamii, na bila shaka wanafunzi wa Ramani Huria.  Profesa Evaristo Liwa, Makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Ardhi, alitoa neno la ufunguzi akianza kwa kueleza kazi iliyopita ya Ramani Huria - Mradi ambao ulifanikiwa kutengneza ramani za kata 21 katika jiji, makazi ya takribani watu milioni 1.3. Alibainisha kuwa awamu…Read more

Kuwafikia Wanajamii kwa Ajili ya Kutengeneza Ramani za Kiwango cha Mafuriko- Kata ya Hananasif

Moja ya kazi ya msingi ya Ramani Huria ni ku tathmini kiwango cha mafuriko Dar es Salaam -na ushiriki wa wanajamii ni kitovu cha shuhuli hii. Nikupitia ushiriki huu ndipo tumepata ujuzi wa ndani na kuongeza kwa kina kiwango cha kutambua maeneo hatarishi ambayo yanaweza kutolewa na jamiii yenyewe. Kutumia taarifa zilizokusanywa, tuna uwezo wa kuunda mfululizo - kuendeleza uwezekano wa kutambua mwenendo wa kihistoria wa kiwango cha mafuriko jijini Dar es Salaam. Kupitia njia hii, tunaweza kuchunguza jinsi hali ya mafuriko ilivyobadilika mwaka hadi mwaka, na ushirikiano wa wanafunzi na wanajamii ni…Read more

Sanaa ya Ramani za Mifereji ya Maji Dar es Salaam 

Moja ya malengo makubwa ya Ramani Huria 2.0 ni kuongeza juhudi zilizofanyika kwenye ramani za mifereji zilizofanyika wakati wa majaribio ya mradi. Wanafunzi sasa wamegawanywa katika makundi mbalimbali ili kurahisisha uratibu na kuwapanga kulingana na ujuzi.Makundi haya ni pamoja na; Timu ya mifereji, Timu ya GIS, Timu ya  Open map kit,Timu ya kuwafikia wana jamii,na timu ya kutengeneza ramani za mbali.(bila kuwa sehemu husika) Hakukuwa na njia inayojulikana ya kutegeneza ramani za mifereji, Hivyo timu  yetu ilibidi kujaribu njia mbalimbali zinazofahamika za kutengeneza ramani, baada ya kujaribu, Kipengele cha Geotrace pamoja na uwezo…Read more

Kudhibiti Ubora Katika Kutengeneza Ramani za Mbali

Kupanua mradi wa kutengeneza ramani kwenye mji wenye watu zaidi ya milioni tano unahitaji mipango na mafunzo sahihi. Tulipenda kwanza wanafunzi wetu wapate  maelezo ya kina ya jinsi taarifa inaingizwa kwenye OSM ili kuhakikisha uelewa wazi wa mazingira ya OSM na jinsi inavyofanya kazi. Katika hatua ya baadaye, tutawaonyesha jinsi taarifa ya OSM inaweza kutumika kwa madhumuni kadhaa tofauti. Kufundisha wanafunzi mia tatu kutengeneza ramani, huja na changamoto kadhaa. Wanafunzi  wetu wote ndio wanaanza, na wengi wao hawajawahi kuchangia kwenye OSM kabla. Kazi yao ya kwanza ilikuwa rahisi- kufungua akaunti za OSM, kusainiwa…Read more