Lengo la Ramani Huria ni ustahimilifu: Kupunguza athari za mafuriko kwa binadamu. Njia ya kawaida kabisa ya kupunguza hili ni ni kuondoa uwezekano wa mafuriko! Mifereji ni moja ya njia ya kufanya hili.

IMG_1483.JPG
IMG_1492.JPG

Culvert                                                          Concrete Drain

ff40e47d-920f-441f-9bad-399dd3d5dd70.jpg
silt.jpg

Ditch                                                                             Silt Trap  

Mfumo wa mifereji ya maji  Dar es Salaam ni mkubwa na mgumu, mamia na maelfu ya mifereji mara nyingi kando ya barabara, Mara nyingi zinaanzia urefu wa mita tatu mifereji ya kujengwa pembeni ya barabara hadi sentimeter tano za mifereje iliyochimbwa na watu wenyewe kutoka kwenye makazi yao. Kusaidia kupunguza mafuriko, tunaweza kutengeneza ramani za mifereji na kuchambua katika programu maalumu ya ufanisi wa hydrolojia. Hii inaweza kutusaidia kujua tatizo na sehemu ambayo inahitaji marekebisho, kuundwa upya au kusafishwa tu na wana jamii. Ili kuchambua mifereji ya maji, tunahitaji zaidi ya mistari kwenye ramani. Tunahitaji wasifu (Sura), vipimo, urefu, aina ya vifaa, na mwonekano wa mfereji. Hata hivyo programu hii ya hydrolojia inahitaji kila kipande cha mfereji kwenye ramani kiunganike, kisikosekane kitu na chochote kisikae vibaya (Kila kitu kikae kwenye sehemu yake ili kuwezesha programu hii kufanya kazi)

Aina hii ya ramani imekwisha kuwa kuhifadhiwa na watafiti wenye ujuzi sana kwa kutumia vifaa vya gharama kubwa. Hata hivyo Ramani Huria imeona fursa ya kufanya kazi na wanafunzi wenye uwezo mkubwa kutoka chuo kikuu cha Ardhi pamoja na wana jamii wenye uelewa wa maeneo yao wanayoishi. Muunganiko huu umesababisha ukusanyaji wa taarifa kwa kiwango kikubwa, na kujikita sehemu nyingi zinazokumbwa na mafuriko Dar es Salaam.

IMG_2386.JPG
IMG_1021.JPG

        PICTURE: Measuring Sticks and Tapes, Showing Hinge on Measuring Sticks.

Kwanza tulianza kwa kuunda fimbo maalum, ili kupata vipimo vya mifereji kwa usahihi (Kwa hakika bila kutumia muda mrefu kuvitengeneza) na kununua tape (futi). Hata hivyo, Licha ya kuwa simu zetu zinapokea GPS, Hatukujua programu yenye suluhisho ambayo ingeturuhusu sisi kuchukua mistari kwa usahihi iwezekanavyo, pamoja na kuchukua vipimo mbalimbali kwenye muundo uliopangiliwa.

Programu tulizopata zilikuwa kwenye makundi mawili;

  • Programu zinazo jikita kwenye kurekodi mistari ya GPS, na
  • Programu zinazo jikita kwenye kuingiza taarifa.
Screenshot_2017-10-26-15-27-19[1].png

                      SCREENSHOTS: Various Android Mapping Applications

Hatukupata chochote ambacho kiliweza kufanya haya yote kwa usahihi. Programu nyingi za Android zinamruhusu mtumiaji kukusanya kiwango kikubwa cha taarifa za mistari ya GPS zenye ubora (Ndani ya kiwango cha ubora wa GPS), ikiwepo ramani inayoonyesha sehemu mtu alipo, uwezo wa kuimarisha ikiwa mstari unapoteza usahihi sehemu moja kwa moja, na uwezo wa kuchuja pointi ambazo hazijakidhi  vigezo sahihi.

data.JPG
dataww.JPG

SCREENSHOTS: OpenDataKit with Various Data Types

Programu nyingine, Hasa OpenDataKit (ODK) ambayo tunaitumia kwa kiango kikubwa wakati wa kuchukua taarifa, inamruhusu mtumiaji kujaza aina maalum ya fomu. Form ya ODK inaweza kuchukua namba ( tarakimu au desimali), maandishi, chaguo kutoka kwenye orodha (chaguo moja au “radio button”, au chaguo nyingi kwa kuchagua kila kinachotumika) na hata picha kutoka kwenye kamera ya simu. Hata hivyo kipengele cha GPS cha kuchukua mistari inapingwa na kuchukua mstari mmoja, haikujitosheleza kabisa. Pale ambapo GPS haikupata satelite , ODK itaanza kutumia pointi ya eneo la mtandao (iliyokokotolewa kutoka kwenye minara ya simu iliyokaribu) ambayo iko mbali kwa mamia au hata maelfu ya mita ( hii ilisababisha mistari iliyochorwa kuruka mbali na haikuweza kutumika kutengenezea ramani).matatizo mengine yalihusisha kutokuwa na uwezo wa kuchagua kizingiti/sehemu kwa usahihi, huwezi kufuta labda pointi chache za mwisho (inakubidi uanze upya pale ambapo kitu hakipo sawa), hakuna njia ya kuonyesha kwa karibu sehemu ambayo mtu yupo,  na muundo wa matokeo ambao haukuwa na upeo na taarifa ya usahihi (zote zinapatikana kutoka kwenye mpangilio wa GPS).

Uchaguzi wetu ulikuwa:

  1. Kutumia programu ya ramani kama vile ya OSMAnd,  ya bure na ya wazi kabisa,na kurekodi taarifa yote katika sehemu  moja ya “maoni”. Hii itahitaji mafunzo na usimamizi mkubwa ili kuhakikisha kuwa taarifa zote zinakusanywa kwa mtindo thabiti.
  2. Kutumia programu ya kuingiza taarifa kama ya ODK yenye uwezo mdogo wa kuchukua mistari, na kuzingatia mapungufu yake.Hii ingeweza kusababisha wachunguzi kutumia muda mwingi kuchukua kila mstari kutokana na kulazimishwa kurudia tena, na utaweza kusababisha matokeo mabovu ya mstari mzima.
  3. Kutumia programu  moja kurekodi mistari, na nyingine kuingiza taarifa, hii itahitaji uhifadhi makini ili kuhakikisha kuwa taarifa zimeingizwa kwenye kwenye mstari sahihi. Wakati wowote taarifa na mistari zikiwa nje ya utaratibu, basi seti nzima ya taarifa itakuwa haina matumizi na itabidi ikusanywe tena (uwezekano wa siku au wiki nyingine za kazi)
  4. Kutengeneza programu ambayo ni bora kwenye kuchukua taarifa au programu ambayo ni nzuri kwenye kuuingiza taarifa za ramani.

Akaingia Ka-Ping Yee, Mhandisi wa programu mwenye ujuzi wa ajabu mwenyenia kubwa ya kufanya kazi za kibinadamu. Ping alikuwa likizo uingereza wakati tunampigia kumuomba msaada, na alikubali kukaa siku chache Dar ea Salaam akijitolea kufanya kazi na Ramani Huria. Tulitaka kazi yetu imsaidie yeyote kwenye ulimwengu wa kutengeneza ramani za kibinadamu/kijamii, na hivyo tunapendelea kwa kiasi kukubwa kutumia programu huru na za wazi kabisa.

Kwa haraka tulianza mkakati wa kuongezea ubora programu huru ya OpenDataKit (ODK) ili iwe na uwezo wa kuchukua mistari kwa usahihi. ODK kwa miaka mingi imekuwa rasilimali kubwa kwenye miradi ya kidigitali ya kibinadamu, hasa kwa sababu ya uwazi na kujitolea kwa jumuia ya watengenezajiwa programu hii. Tulijua kwamba, ikiwa tutaongeza kazi kwenye ODK, si tu Ramani  Huria ingeweza kufaidika, lakini sekta nzima ya kibinadamu ingeweza kufaidika maboresho yetu.

Kuchangia kwenye programu programu huru /wazi ni ngumu zaidi ya inavyoonekana. Kabla ya kufanya marekebisho kwenye mradi, ni muhimu kuwasiliana na jamii ambayo imeunda na inaendeleza programu hiyo. Kama hili halitafanyika, ni rahiisi sana kurudia kazi ambayo tayari ilishafanyika au hata kufanya marekebisho ambayo  hayatapatana na kuvunja/kuharibu sehemu nyingine za programu. Kwa sababu hiyo, wakati mwingine watengenezaji wa programu za wazi wanakuwa na hisia kali na miradi waliyotengeneza, na wanaweza kujitetea/kujilinda endapo mtu ataingilia mtoto(programu) ambaye wamekuwa wakimpa upendo, muda, na uangalizi, hasa kama wageni wataingia bila kujitambulisha na kuonyesha unyenyekevu kidogo. Zaidi ya hayo, mabadiliko ya programu hayapaswi kufanywa yote kwa mara moja, bali kwa kuingiza mabadiliko kwa kuyatenga, ikihusisha na nyaraka za wazi, kuruhusu kujaribiwa na kuhakikiwa ili isiharibu mambo. Mpangilio wetu wa maboresho ya kificho (code) ya Ping ulifikia mabadiliko kadhaa tofauti, na utahitaji ufungaji kama mtu binafsi (“kiungo”) (kiungo fulani na ufafanuzi wa vitendo vya git) pamoja na majadiliano na diplomasia.

Tuliwasiliana na Helen Martin, moja kati ya watengenezaji wa ODK, na jamii ya ODK kwa kiasi kikubwa walitukaribisha na walifurahushwa na kazi yetu. Ping ali “fork repo” ya ODK, na akaja Tanzania kuanza kazi.

Kulikuwa na matatizo machache makuu yaliyotaka kusababisha ODK karibu isiweze kuchukua taarifa za mistari. Kuruka mara kwa mara kwa point ya GPS kwa sababu ya mtandao, kutokuwa na uwezo wakuweka kizingiti kwa usahihi, na ulazima wa kuanza mwanzo wakati kitu chochote hakijaenda sawa ndio kubwa zaidi. Ping alianza kwa kuongeza usahihi wa kuchuja na kutengeneza button “backspace” kufuta point za mstari zilizochukuliwa mda huo.( kwa hiyo mtumiaji angeweza kurudi nyuma kwenye baadhi ya pointi na sio kuanza mwanzo).

spreadsheet.JPG

SCREENSHOT: The Prioritization Spreadsheet

Kila siku Ping aliwauliza Sadah na Felix, (Wanaotengeneza ramani za mitaro), Randy Jones (anayejitolea kutoka Canada) na Ivan Gayton (Meneja wa HOT-Tanzania), kuona ni mabadiliko gani yangeweza kusaidia kazi ya timu. Hii ilikuwa uwiano mkali kati ya mabadiliko ambayo yatakuwa na athari nyingi na yale ambayo yatachukua muda mwingi; “mafanikio ya haraka” (athari kubwa na rahisi kutekeleza) ilichosha kwa haraka.

Masuala machache yalitokea kuwa magumu zaidi ilivyodhaniwa. Kwa mfano ODK inahamisha mistari kama mmfululizo wa pointi ambazo hazielezwi na kitu chochote zaidi ya namba nne (Latitudo, Longitudo, Mwinuko  an usahihi wa GPS) uliotenganishwa na koma na mikato mwili katiya pointi). Programu za ramani hazijui nini cha kufanya juu ya mfululizo huu bila muktadha. Kwa hiyo tunabadilisha muundo kwenda kwenye nakala inayojulikana (well known text), mfumo wa taarifa za kijografia za programu za ramani kama QGIS, programu ya ramani ya bure na wazi tunayoitumia ambayo inaweza kutambua na kuonyesha taarifa hizi.

Capture.JPG

SCREENSHOT: Some WKT String Examples

Hata hivyo, tuligundua kuwa hii iliivunja/haribu ODK! Wakati wowote mtumiaji akijaribu kufungua  tena dodoso baada ya kulihifadhi, mistari ya nakala nakala inanyojulikana inapotea. Inabadilika kuwa lugha ya ufafanuzi wa fomu ambayo ODK imekataa, Javarosa ina sarufi maalum kwa ajili ya mistari – mfululizo uliotajwa hapo juu wa namba nne zilizoteuliwa na koma mbili kati ya pointi – ambazo haziendani na Well Known Text (au muundo wowote wa kijiografia ambao tunajua). Bila kufanya marekebisho makubwa kwenye Javarosa (ambayo kwa kweli ingevunja mambo mengine,  hasa kwa watu wa mbali ambao hawawezi kujua nini tumefanya, na wangetuchukia wakijua tulichofanya), hatukuweza kutekeleza vifungo vya nakala zinazojulikana viizuri katika ODK. Tulipaswa “kurekebisha mabadiliko” na kurudi kwenye utekelezaji wa awali ambao hutoa taarifa ambazo haziwezi kufunguliwa katika programu ya ramani. Kutatua, au angalau kupunguza hii Ping aliandika [Plugin utility plugin] (github.com/zestyping/THE LINESTRING PLUGIN) kwa QGIS kubadili mistari ya Javarosa katika nakala inayojulikana vizuri.

Screenshot_2017-10-26-15-40-57.png

SCREENSHOT: The New ODK Line Trace Interface

Mabadiiliko mengi ya kiufundi baadae, tuliishia kujadili kitu kingine kipya kabisa: Wataalam wa ramani pale chuo cha Ardhi walivyojaribu kuangalia taarifa walizokusanya kwenye compyuta waligundua kuna baadhi ya pointi na vipande havionekani. Wataalam hawa , mbali na juhudi walizozifanya hasa Sadah, Randy na Feliix, baadhi ya taarifa zilikosekana, ilikuwa adimu, lakini taarifa za nyingi zilitumwa kwa mtaalamu wa hydrologia hazikukamilika na nyingine hazikuungana. Wasimamizi walishindwa kujua  kama taarifa zote zimechukuliwa, na walitakiwa kusubiri hadi wataalam wa ramani waangalie kwenye compyta wakiwa chuo. Tuliwaza ‘’Vipi kama wataalam na wasimamizi wanaweza kuona vipande vyote na pointi kwa mda sahihi, ili waweze kujua kitu gani hakijachukuliwa kabla ya kuondoka kwenye eneo. Kwa hiyo Ping alitengeneza kitu kingine, alitengeneza portal kwenye mtandao ambayo ingemwezesha msimamizi wa ramani kuona pointi na mistari kwenye mtandao (simu au compyuta) kabla ya kuondoka kwenye eneo la kukusanya taarifa.

Kobo view.JPG
Screenshot_2017-10-26-15-44-48.png

            SCREENSHOTS:     Kobo Viewer on Laptop            Kobo Viewer on Phone

Hatimaye, tuna suluhisho la programu yenye uwezo wa kuchukua mistari ya GPS kwa kiwango cha usahihi na ufanisi tunaohitaji, uwezo wa ajabu wa ODK kuingiza aina sahihi za taarifa, na chombo cha usimamizi  cha kusimamia timu kukamilisha kikamilifu kazi ya ukusanyaji taarifa za ramani. Hata hivyo bado sio mda wa kusherehekea, bado kuna vitu vingi vya kufanya.

“Fork” na mabadiliko yetu yote kwenye ODK bado haijaunganishwa kwenye “codebase” kuu ya ODK (majadiliano na jamii ya ODK inaendelea, na kazi zaidi inapaswa kufanyika kwenye nyaraka na ufungaji). Tumetengeneza ramani saba za Dar es Salaam kwa kutumia njia zetu, lakini sehemu ndogo tu ya ramani imethibitishwa na wataalam wa programu ya hydrologia nchini Uholanzi; tunahitaji kuhakikisha kuwa kazi yetu inafaa kikamilifu kabla ya kuanza kutengeneza ramani za mji wote. Mwishoni, tunahitaji kuandika kazi yetu yote, kuifunga, na kuandaa kitabu kwa  mtu mwingine yeyote ulimwenguni ambaye anaweza kuboresha mifereji ya mijini kupitia ramani za jamii!

Kipindi Ping anafanyia kazi programu, Randy Jones, aliyejitolea kutoka Canada kuongoza timu ya wanaotengeneza ramani za mifereji mwezi wa mwanzoni, anatengeneza  Wiki-based playbook for practical community-based urban drainage mapping  kulingana na njia ambazo tumeanzisha Dar es Salaam na Ramani Huria. Tunatarajia kazi ya Ramani Huria itafaidisha idadi kubwa ya watu ulimwenguni kote walio kwenye hatari ya mafuriko. Timu yetu hapa hapa Tanzania itaongoza njia!

Leave a Reply