Tarehe 26 Septemba 2017, ukurasa mpya wa RAmani Huria 2.0 ulifunguliwa rasmi kwenye ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Tukio lilihudhuriwa na wadau muhimu wakiwemo maafisa wa serikali, maafisa wa vyuo vikuu, Washiriki kutoka kikosi  cha msalaba mwekundu, wataalamu wa ramani, wana jamii, na bila shaka wanafunzi wa Ramani Huria. 

Profesa Evaristo Liwa, Makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Ardhi, alitoa neno la ufunguzi akianza kwa kueleza kazi iliyopita ya Ramani Huria – Mradi ambao ulifanikiwa kutengneza ramani za kata 21 katika jiji, makazi ya takribani watu milioni 1.3. Alibainisha kuwa awamu hii iliyopanuliwa inatarajiwa kufikia makazi ya zaidi ya watu  milioni tatu wa Dar es Salaam, Mara mbili ya mradi wa mwanzo wa majaribio

Risala ya Profesa Liwa ilijikita kwenye umuhimu wa ushirikiano kwenye mradi huu – akionyesha ushirikano kati ya chuo kikuu cha  Ardhi na benki ya dunia ambao hadi sasa wameweza kuhamisha ujuzi na maarifa ya usimamizi wa athari za maafa kwa wanafunzi zaidi ya mia nne. ‘’Kupitia msaada kutoka benki ya dunia na mradi wa Ramani Huria, wahitimu wengi wa Chuo Kikuu cha Ardhi wamekuwa wataalamu na kuajiriwa katika sekta mbalimbali,” alisema.

IMG_1823.JPG

 Profesa Evaristo Liwa- Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Ardhi akifungua warsha

Bwana Michael Ole-Mungaya, mwakilishi wa katibu tawala mkoa-Dar es Salaam alifuata kuupa sifa mradi, sasa Ramani Huria ni kampeini kubwa ya ramani za jamii duniani. Alianza kwa kubainisha kuwa Dar es Salaam ni jiji linalokua kwa kasi na ongezeko la tatizo la ukusanyaji taka, moja kati ya vitu vinavyochangia mafuriko. Kufuatia hili, alisisitiza kwamba msaada kwa Ramani Huria unaendelea kutoka pande zote, kwa njia ya ushirikiano huo tunaweza kufanya mji wetu kuwa na nguvu zaidi.

Mkurugenzi wa benki ya dunia – Tanzania, Bi Bella Bird, alitukumbusha zaidi kwamba Tanzania ni waathiriwa zaidi wa mafuriko Afrika Mashariki, na kwamba mzigo huu unaongezwa sana na idadi ya watu kutoka kwa mtazamo wa kijamii na kiuchumi. Alisisitiza umuhimu wa kupanua mradi kama Ramani Huria na alikuwa na furaha kuripoti kwamba Benki ya Dunia haitacha msaada wake.

Picha ya pamoja ya washiriki

“Nini sababu ya mpango Ramani Huria kuwa wa kipekee” Thomas Allen Naibu Mkuu wa Idara ya  Maendeleo ya Kimataifa – Uingereza (DfID), aliendelea “Ni vijana na ubunifu” Kama alivyoongea Bi Bella , bwana Allen aliongeza kuwa Uingereza inafurahia kuunga mkono mpango huu katika lengo lake kuu la kuboresha ustahimilifu wa miji nchini kote.

Mwishoni mwa warsha, Mkataba wa makubaliano ulisainiwa kati ya chuo kikuu cha Ardhi, benki ya dunia na DfID kama makubaliano rasmi ya kuongeza ushirikiano kati ya wadau hawa na kuboresha upatikanaji wa elimu ya vitendo kwa vijana juu ya usimamizi wa athari za maafa 

Kutia sahihi mkataba wa makubaliano

Baada ya picha za pamoja za kusherehekea, washiriki walikaribishwa kwenye maonyesho ya kazi ambayo Ramani Huria imekuwa ikifanya hadi sasa – ambazo ni kutengeneza ramani za mifereji, ramani za kiwango cha mafuriko, ramani za miundombinu, na hatua za dharura.

IMG_1904.JPG

Maonyesho

Leave a Reply