Moja ya kazi ya msingi ya Ramani Huria ni ku tathmini kiwango cha mafuriko Dar es Salaam -na ushiriki wa wanajamii ni kitovu cha shuhuli hii. Nikupitia ushiriki huu ndipo tumepata ujuzi wa ndani na kuongeza kwa kina kiwango cha kutambua maeneo hatarishi ambayo yanaweza kutolewa na jamiii yenyewe.

Kutumia taarifa zilizokusanywa, tuna uwezo wa kuunda mfululizo – kuendeleza uwezekano wa kutambua mwenendo wa kihistoria wa kiwango cha mafuriko jijini Dar es Salaam. Kupitia njia hii, tunaweza kuchunguza jinsi hali ya mafuriko ilivyobadilika mwaka hadi mwaka, na ushirikiano wa wanafunzi na wanajamii ni muhimu kwa uzalishaji wa taarifa na ustawi. Baadaye kukamilika kwa tafiti zitategemea muungano kati ya wana jamii na mradi huu.

Jinsi kazi ilivofanyika  

Baada ya kukutana na viongozi wa ngazi ya mtaa,wanafunzi wanaenda nyumba hadi nyumba kuelezea mradi kwa wanajamiii, kama mwananchi atavutiwa, basi mwanafunzi atamuonyesha jinsi ya kutumia programu ya Opendatakit Collect (ODK) na kuwaeleza jinsi ya kujaza utafiti kwa usahihi. Vocha za simu na motisha ya fedha hutolewa kwa wale wanaofanya uchunguzi, kama chanzo cha motisha kwa ushiriki wa jamii katika kufanya kazi na sisi.

Wana jamii wapya hupelekwa kwenye mto na wanafunzi na kuelekezwa jinsi ya kutumia programu. Kutoka pointi/sehemu waliyosimama kwenye mto, wanajamii wanaelekezwa kutembea moja kwa moja mbali na mto ili kuchunguza/kutafiti nyumba njiani – kutambua kama wanapata au laa. Mwanafunzi anaambatana na mwana jamii kwenye nyumba 1 au 2 na kisha anamuacha mwana jamii huyo kuendelea mwenyewe ili kukamilisha utafiti huo. Hii hutumiwa kama mbinu ya kukusanya taarifa wakati mtu anatembea. (transect-like data collection methodology).

ttttttttttttttttttttttttttttttttt.JPG

Mwanafunzi akimuelezea mwanajamii jinsi kazi inavfanyika

Mara baada ya mwana jamii kurudi, Mwanafunzi atasimamia mbadilishano wa maarifa kati ya wanajamii wenyewe. Mwanajamii aliyerudi sasa anakuwa mwalimu na kusaidia kuwaunganisha wananchi wengine kwenye shuhuli hii.

Changamoto

Shuhuli/kazi hii bila shaka ina baadhi ya changamoto. Kuligundulika mapema kuwa baadhi ya maswali ya utafiti yalifafanuliwa vibaya, kwa mfano.’umewahi kupatwa na mafuriko?’ Wanajamii wengine walijibu kupatwa na mafuriko kupitia anuani zilitopita( makazi mengine ambayo walikuwa wakiishi hapo kabla). Kuandika tena na kufafanua utafiti huu kwa baadhi ya wanajamii kulifanyika na wanafunzi waliendelea kufanya mafunzo zaidi.

Baadhi ya wana jamii wamekuwa wakisita kushirikiana kwa sababu ya kutoaminiana /kutokuwepo kutambuliwa kwa wachunguzi wanafunzi. Hili suala  tumelishughulikia kwa kutoa barua za utangulizi kuhusu mradi.

Wanajamii wengine wamehama  nyumba kwa sababu ya matukio ya mafuriko na , hivyo baadhi ya pointi za GPS haziwezi kuwekwa kama kumbukumbu za mafuriko. Inaweza kuwa zoezi la kuvutia kujua ni watu wangapi wamehama kutokana na mafuriko ili kuona jinsi gani mafuriko yameathiri idadi ya watu.

Matokeo

Licha ya changamoto hizi, namba ya tafiti zilizofikiwa ni zaidi ya tulivyodhani kuwa inawezekana. Ukuaji wa namba za utafiti umekuwa mkubwa sana – kuanzia tafiti mia moja tu kwa siku moja hadi zaidi ya 840  kwa siku moja, ukuaji uliofanyika ndani ya siku 8 tu. Hii sio tu inathibitisha jinsi ushiriki wa jamii unavyo zaa matunda , bali ni kwa kiasi gani tuna uhakika wa kusonga mbele. Mashaka yote ya awali juu ya lengo la mradi yamemalizwa na kupanda kwa takwimu hizi za uchunguzi, Hii inaonyesha kwamba kiwango kikubwa zaidi kitafikiwa. Hadi sasa, tuna tafiti zaidi ya 1000 zilizokamilika.

Kwa ongezeko la msaada kutoka kwa wanajamii, tuliwachukua wanajamii nane (kutoka Hananasif na Kawawa) kuja mtaa wa Mkunguni ‘A’ kuona jinsi gani tunashirikiana na viongozi wa mtaa. Kufuatia utaratibu uliowekwa na wanafunzi kwenye kata ya kwanza tuliyozuru, Wamajamii walishirikiana kikamilifu na viongozi wa mtaa, kuuliza kuhusu mipaka ya mtaa na kuuliza kuhusu eneo hilo.Pia tuliandaa kikao na wanajamii pamoja na viongozi wa mitaa, tunatambua kuwa kuimarisha uhusiano huu kutafanya mradi kuwa endelevu.

commmmmmmmmmmmmmmmmmm.png

Kikao na Viongozi wa Mitaa

Katika mchakato huu, Imegundulika kuwa mifereji mibovu na iliyoharibika kunachangia mafuriko kwa kiasi kikubwa kwenye maeneo yaliyopo mbali na mto. Sababu hizi zimegundulika kupitia wanafunzi kuwashirikisha wanajamii kikamilifu – baada ya kuangalia taarifa hizi na kuonyesha kwa pamoja sehemu ambazo si rahisi mafuriko kutokea. Hii ndiyo sababu kushughulikia mafuriko ni suala gumu sana ambalo linahitaji ushirikiano mkubwa kati ya watendaji husika, timu ya Ramani Huria ni kati yao.

Leave a Reply