Moja ya malengo makubwa ya Ramani Huria 2.0 ni kuongeza juhudi zilizofanyika kwenye ramani za mifereji zilizofanyika wakati wa majaribio ya mradi. Wanafunzi sasa wamegawanywa katika makundi mbalimbali ili kurahisisha uratibu na kuwapanga kulingana na ujuzi.Makundi haya ni pamoja na; Timu ya mifereji, Timu ya GIS, Timu ya  Open map kit,Timu ya kuwafikia wana jamii,na timu ya kutengeneza ramani za mbali.(bila kuwa sehemu husika)

Hakukuwa na njia inayojulikana ya kutegeneza ramani za mifereji, Hivyo timu  yetu ilibidi kujaribu njia mbalimbali zinazofahamika za kutengeneza ramani, baada ya kujaribu, Kipengele cha Geotrace pamoja na uwezo wake wa kuwezesha utengenezwaji wa tafiti zilizoboreshwa, iliwekwa na ODK pamoja na programu zote zilizojaribiwa. Hii ni programu ya simu ya mkononi (Android) ya bure na ya wazi ambayo husaidia mashirika kukusanya taarifa na kusimamia ukusanyaji wa taarifa kwa kutumia simu ya mkononi. Form ya kukusanya taarifa hutengenezwa (XLS Forms inashauriwa kwa ukusanyaji wa taarifa nyingi) na ukusanyaji wa taarifa unafanyika kwenye simu ya mkononi. Kisha hutuwa kwenye seva ambayo inaunganisha taarifa na kufanya ipatikane kwenye mifumo mbalimbali kwa ajili ya matumizi.

Baada ya kutengeneza/kuunda fomu sahihi, Wanafunzi walifundishwa jinsi ya kutumia ODK kwenye simu zao.  OSMAnd ni programu nyingine inayowasaidia wanafunzi kuwa na mwelekeo sahihi wakati wanazunguka kutengeneza ramani jijini, Na kazi ya GeoTrace inasaidia sana kwa ramani ya mifereji na makalavati kwa kuchukua pointi kwa usahihi wakati mwanafunzi anachukua taarifa ya kitu husika.

.

Mwanafunzi akichora mtaro

Kwa kuongeza, Wakati wa kukusanya taarifa, wanafunzi wanatumia ODK kuchukua pointi kwa usahihi kando ya mfereji. Pointi hizi ni pamoja na mwanzo wa mfereji, Mfereji ulipoharibika au kufungwa, Sehemu ambayo mfereji unaungana na mali binafsi, Sehemu ambayo mfereji umeingia, Sehemu mfereji unapotoka na nyingine nyingi.  

Ili kupata vipimo sahihi vya taarifa mbalimbali za mitaro au makalavati, zana zinazofaa kwa kusudi hili zilihitakiwa. Ilihusisha vifaa kama utepe wa kupimia (Tape measure), kutumia fimbo iliyotengenezwa kwa vipimo (iliyoundwa na timu yetu ya tanzania) kupima urefu na upana wa mitaro pamoja kipenyo cha kalavati. Takwimu za mifereji ya maji zinahitajika kupimwa kwa usahihi kwa kuwa lengo la Ramani Huria ni kuboresha ustahimilivu wa mafuriko kwenye jiji, na mirereji ina mchango mkubwa katika hili.

IMG_1129.JPG

Wanafunzi wakipima kina cha mtaro kwa kutumia fimbo iliyotengenezwa kwa vipimo

Kwa majaribio ya uelewa wa wanafunzi katika mchakato huu wa kutengeneza ramani tuliwapeleka kata ya Hananasifu kwa ajili ya kukusanya taarifa. Wanafunzi walijigawa wenyewe katika makundi kulingana mitaa kisha wakatanwanyika kukusanya taarifa. Mchakato ulikua na changamoto kadhaa kwasababu ilikuwa ndo mara ya kwanza kwa wanafunzi hawa kukusanya taarifa rasmi za mitaro na baadhi ya wanajamii walitazama mchakato kama ni wa kisiasa, lakini wanafunzi walikua makini kuelezea lengo la mradi wa Ramani Huria kwa mtu yoyote alichunguza. 

Changamoto nyingine iliyojitokeza ni uelekeo wa maji katika mitaro. Wakati mwingine ni vigumu sana kuona upande upi maji yanaelekea. Tatizo hili lilitatuliwa kwa kuwauliza wanajamii kuhusu uelekeo wa mtaro husika au kwa kutizama kwa umakini katika mkusanyiko wa mchanga na uchafu.

Pia kulikuwa na changamoto ya usahihi wa mifumo ya GPS za simu za mkononi. Baadhi ya changamoto hizi zilitatuliwa na mtaalamu wa programu za kompyuta, Ka-Ping Yee kutoka nchini Marekani lakini kwa baadhi ya maeneo yalibaki kuwa tatizo, wakati wa upokeaji wa usahihi wa pointi ya GPS kwenye simu za mkononi.       

Mara kwa mara wanafunzi walikutana na upizani kutoka kwa wanajamii ambao hawakufahamu vizuri kuhusu mradi. Suala hili linaonyesha kwanini Ramani Huria ina msisitizo mkubwa katika uhusishwaji wa wanajamii.

Wanafunzi Wakiwa kata ya Hananasif

Licha ya matatizo machache, Wanafunzi walikusanya taarifa nyingi wawezavyo. Ripoti yao inaonyesha kuwa kuna mitaro mingi ambayo haijaungana, Mitaro yenye taka, na mitaa mingine haikuwa na mitaro kabisa-yawezekana kuwa ndio chanzo kikubwa cha mafuriko mabaya. 

Taarifa zilizokusanywa kwenye maeneo haya zinachambuliwa kwa usahihi kutumia programu ya QGIS. Wakati wa kuangalia data kupitia programu hii baadhi ya makosa yalijitokeza kama vile taarifa zilizokosekana na ambazo hazikuwa sahihi. Kwa kesi kama hizi, wanafunzi walienda kukusanya tena taarifa. Wakati mchakato unaendelea, wanafuzi wanaendelea kuelewa umuhimu wa kuangalia ubora wa taarifa wakati wa ukusanyaji

kisutu3.png

       Taarifa za mitaro ya Mtaa wa Kisutu Kata ya Hananasif  zikionyeshwa kwenye QGIS

Waanfunzi wetu wataendelea na mafunzo ya vitendo ili kuhakikisha wanakuwa na ujuzi unaohitajika wakati wa kufanya mchakato rasmi wa kutengeneza ramani.

Leave a Reply