Kupanua mradi wa kutengeneza ramani kwenye mji wenye watu zaidi ya milioni tano unahitaji mipango na mafunzo sahihi. Tulipenda kwanza wanafunzi wetu wapate  maelezo ya kina ya jinsi taarifa inaingizwa kwenye OSM ili kuhakikisha uelewa wazi wa mazingira ya OSM na jinsi inavyofanya kazi. Katika hatua ya baadaye, tutawaonyesha jinsi taarifa ya OSM inaweza kutumika kwa madhumuni kadhaa tofauti.

Kufundisha wanafunzi mia tatu kutengeneza ramani, huja na changamoto kadhaa. Wanafunzi  wetu wote ndio wanaanza, na wengi wao hawajawahi kuchangia kwenye OSM kabla. Kazi yao ya kwanza ilikuwa rahisi- kufungua akaunti za OSM, kusainiwa ili kujiunga na jamii ya kimataifa ya wachagiaji, tuliwaingiza kwenye jukwaa la OSM na kuwaonyesha jinsi ya kuhariri.

Moja ya malengo ya Ramani huria 2.0 ni kutengeneza ramani za jiji zima la Dar es Salaam kwenye OSM. Tulianza kwa kuwagawanya wanafunzi wetu kwenye makundi manne na kuwagawia kazi za ramani. Katika masaa machache, kazi ndogo sana zilifanywa  kwa asilimia mia moja, na wanafunzi walielekezwa kwa ufanisi jinsi ya kutengeneza ramani na walifanikiwa kuchangia kwenye OSM.

Tulitarajia wanafunzi wanaweza kusababisha makosa mbalimbali, na kweli ilikuwa hivyo – Ubora wa taarifa.

Jioni ile, tulipata ujumbe kutoka kwa moja kati ya wataalamu wenye uzoefu kwenye jamii ya OSM, ikionyesha baadhi ya makosa yaliyofanywa na wanafunzi wetu. Hii ndiyo nguvu ya jamii ya OSM. Mwanzoni wakati wa mafunzo, Swali liliulizwa kuhusu uhalisi wa taarifa za OSM na jinsi makosa yanavyotatuliwa na kudhibitiwa. Hili ndilo jibu, Jamii daima inaangalia taarifa hizi.

Wanafunzi wakichora ramani kutumia JOSM.

Kisha kwenye ajenda yetu ilikuwa kushughulikia maswala haya ya ubora wa taarifa, ambayo ni hatua muhimu katika kuchangia kwa ufanisi kwenye OSM. Masuala makuu yaliyotambuliwa yalikuwa makosa ya maandishi, majengo yasiyo na majina/sifa na majengo kadhaa ambayo hayajachorwa kwa ufasaha au majengo kushikamana. Tulitaka kuanzisha njia rahisi za kukabiliana na hili wakati pia tukitumia fursa ile ile kuonyesha thamani ya zana zaidi katika JOSM.

Josm filter ilisaidia kutatua changamoto za ubora wa taarifa, kwa mwongozo wa plugin kama orodha ya Todo. Mchanganyiko wa mambo haya ulituleta karibu kabisa katika kuondoa tatizo hilo. Timu zilihakiki kazi, ambazo zilipunguza na kuondoa baadhi ya makosa haya, lakini baadhi ya makosa hayakutatuliwa.

Kazi mpya ilianzishwa baadaye, iliyolenga  kuthibitisha taarifa ambayo iliundwa hapo awali.

Kazi mpya iliyotengenezwa.

Hatua za hili ni kama zifuatazo.

 • Chagua eneo la kuhakiki na fungua kwenye JOSM.
 • Tumia picha ya anga ya bing kuhakiki,kama inamawingu tumia Mapbox au DigitalGlobe Premium.
 • Angalia kama majengo yote yamechorwa kwenye sehemu unayofanyia kazi,kama kuna majengo ambayo hayajachorwa, yachore vizuri na yaandike building=yes.
 • Tumia filter kuficha barabara, matumizi ya ardhi, njia za maji. Ongeza filter zifuatazo kwenye JOSM.
 • type:node untagged (kuficha nukta zote ambazo hazina majina).
 • highway=* (kuficha barabara).
 • waterway=* (kuficha njia za maji).
 • landuse=* (kuficha matumizi ya ardhi).

Kutumia filters

 • Tumia Todo list plugin kuangalia sifa za jengo moja baada ya jingine.
  • Sifa za kuangalia ni;
   • building=yes                                          
 •  Makosa mengi yalikuwa yafuatayo;
  • buildin=yes
  • BUILDING=yes
  • Building=yes
  • building:=yes
  • builging=yes
  • bulding=yes
  • biuilding=yes
  • bubuilding:=yes
  • buildind=yes
  • builing=yes

Majengo yameongezwa kwenye orodha ya Todo ili kuchunguzwa 

 • Majengo yakisha hakikiwa (umbo na jina/sifa), thibitisha na angalia kama kuna kosa lolote na rekebisha.
 • Pakia kwenda kwenye OSM

Hatua hizi zilisuluhisha masuala kwa kiasi kikubwa. Hata hivyo, kulikuwa na baadhi ya makosa yaliyobaki hata baada ya kuangalia kazi tena. Tatizo sasa halikuwa lililohusiana na uendeshaji wa kazi, lakini kwa uzoefu. Wanafunzi wetu wanahitaji muda zaidi wa kufanya mazoezi ya kuchora  ramani ili kupunguza baadhi ya makosa haya ya ufanisi.

Tunazingatia pia kama swala la maandishi linaweza kuwa kipengele muhimu kwenye JOSM! Wachora  ramani mengi, hususan wapya, hufanya shughuli ndogo, kama vile kuongeza majengo; Wao mara chache huhutaji majina mengine ya kuweka nje ya majina ya msingi  ya kawaida ya OSM. Pengine JOSM ingeweza kuwakumbusha wachora ramani wakati lebo/jina lisio ndani ya JOSM (labda kutokana na makosa ya kimaandishi)? 

Kuna mtu/mtaalam yeyote kwenye jamii anataka kuangalia hili?

Leave a Reply