Timu mpya na iliyoongezwa ya Ramani Huria 2.0, yenye hadi zaidi ya wanafunzi mia tatu, kwa sasa ipo katika mazoezi ya vitendo ya kukusanya taarifa na kuhariri ramani ya kidigitali ya Dar es Salaam.

Tumeweka OpenDataKit (ODK), programu huru inayotumika kukusanya taarifa kwenye simu za smatifoni. Tutatumia mitandao mingine ya kisasa zaidi katika kukusanya taarifa kama vile OpenMapKit, programu ya haja ya ODK ambayo inaruhusu maingiliano ya moja kwa moja na taarifa za OpenStreetMap, lakini programu ya kuheshimika na yenye nguvu ya ODK ni nzuri kwa kuanzia. Tulianza kwa kufanya mazoezi ya vitendo kwenye viwanja kuzunguka dLab.

IMG_0431.JPG

Wanafunzi wakitumia ODK kwenye eneo la dLab.

Kwa kutumia ODK mtu yeyoye anaweza kuchukua pointi za GPS katika usahihi mzuri, na ya kutosha kwa aina nyingi za tafiti na pia kurekodi kwa kisasa majibu mengi kutoka kwenye utafiti ikiwemo maandishi, namba, machagulio kutoka kwenye orodha ya chaguzi, na hata pia picha! Uwezekano wa kukusanya taarifa iliyopangwa vizuri kwenye simu za mkononi ni ya kushangaza na kufurahisha, na wanafunzi wanashangaa wakati wa kuwaonyesha matokeo ya kazi yao kwenye ramani.

Water tank map at CoICT campus.jpeg

Taarifa za matenki ya maji zilizokusanywa na wanafunzi eneo la CoICT Chuo kikuu Cha Dar es salaam. 

Tuliwatuma wanafunzi nyumbani siku ya Ijumaa wakiwa na kazi ya mazoezi ya utafiti wa nyumbani, tukiwauliza kwenda kwa majirani zao mwishoni mwa wiki na kuuliza mfululizo wa maswali kuhusu aina gani ya nyumba watu wanaishi, kata na mitaa  wanayoishi, kama huwa wanapata mafuriko, jinsi/wapi wanapata maji, na aina ya vyoo wanavyotumia. Utafiti huu ni kwa ajili ya mazoezi ya vitendo (na wanafunzi wanaagizwa kuwaambia majirani zao hili ili kuhakikisha kwamba matarajio yasiyofaa hayaundwi), lakini inayotoa picha ya kushangaza na kufurahisha ya eneo kubwa  la Dar es Salaam. Kwa mshangao na furaha yetu, zaidi ya tafiti 900 zinakamilishwa mwishoni mwa wiki!

Household water sources zoomed image credit OSM.jpeg

Ramani ya Uchunguzi wa Kazi ya nyumbani, Inayoonyesha Chanzo cha Maji ya Kaya

Siku ya Jumatatu, tunatoka kwenye kumbi kubwa na kurudi kwenye madarasa manne Chuo Kikuu Ardhi, ambapo tulianza mafunzo kwa wanafunzi juu ya matumizi ya Java OpenStreetMap (JOSM), programu ambayo inaruhusu mtu yeyote aliye na kompyuta kuongeza taarifa kwenye OpenStreetMap. Ramani Huria ina nia ya kuweka kila jengo lililoko Dar es Salaam kwenye ramani, kwa hiyo tunaanza mara moja kwa kuchora majengo kutoka kwenye picha ya anga. Kuanzia Jumatatu mchana hadi jioni, wanafunzi 204 wenye kompyuta (kwa kusaidiwa na wanafunzi wengine mia moja ambao wanaangalia na kusaidia) waliongeza majengo zaidi ya 16,000 kwenye ramani! Wakati kuweka kila jengo katika mji kwenye ramani ni kazi kubwa, na hatujui kama tutaweza kufanya hivyo, lakini matokeo haya ya awali yanatia moyo sana.

IMG_0721.JPG
tasks coverage.jpeg

Picha ya ramani ya eneo lililochorwa.

Mwanafunzi akichora jengo

Mwishoni mwa siku ya Jumatatu, kwa kuhamasishwa na matokeo ya utafiti wa mazoezi ya wanafunzi, tunaanza jaribio muhimu; Je! Tunaweza kuimarisha wanafunzi wetu mia tatu waweze kutengeneza maelfu ya wana jamii watengeneza ramani? Tunawapatia vocha za simu za mkononi zenye muda wa maongezi, na kuwaelekeza wanafunzi kutafuta watu katika jumuiya zao, kuwapa vocha hizo, na kuwafundisha kupakua na kuweka ODK, na kujaza utafiti wa usajili. Jumanne asubuhi matokeo ya awali yameingia; wanajamii 170 walionyesha uwezo wa kujaza utafiti wa msingi na ODK kwa simu zao wenyewe! Wanafunzi, hata hivyo, hawakuridhika, wakasema kuwa wanaweza kufanya vizuri zaidi ikiwa wana muda zaidi. Leo tutamaliza swala la JOSM mapema na kuona jinsi watakavyofanya  hili.

Ndoto ya Ramani Huria, na kwa kweli ndoto ya miradi ya ramani ya wazi/huru kila mahali, ni kufanya ramani kuwa mchakato/mfumo shirikishi unaohusisha jumuiya nzima, ya kila mtu. Ikiwa wanafunzi wetu watakuwa na uwezo wa kufundisha na kuwawezesha wananchi kukusanya, kuelewa, na kutumia taarifa za mitaa katika jamii zao wenyewe, ni nani anayejua nini tunaweza kukamilisha?

Leave a Reply