Humanitarian Openstreet Team (HOT) na Ramani Huria, wakifadhiliwa na benki ya dunia na wadau wengine wameanzisha safari mpya na Chuo Kikuu Ardhi!

Wanafunzi mia tatu wa Mipango Miji na Geomatics kutoka Chuo Kikuu Ardhi jijini Dar es salaam wanashiriki katika mradi wa kutengeneza ramani za jamii mwezi Julai na Agosti.Tutatengeneza ramani za kata 35  jijini,msisitizo ukiwa katika taarifa zinazohitajika ili kuzuia mafuriko.

Kwa ongezeko la athari za mabadiliko ya tabia ya nchi na ukuaji wa miji, mafuriko mjini yamezidi kuvuruga na kutishia maisha ya watu wa Dar es Salaam. Ili kusaidia watu jijini, tutatengeneza ramani za mitaro, huduma za afya (muhimu kupunguza magonjwa na vifo endapo kutakuwa na mafuriko, hasa kwa watoto), vyoo, vyanzo vya maji, na miundombinu ya majengo.

Pia tutafanya kazi kuelewa wapi mafuriko yalitokea na wapi yanaweza kutokea mbeleni kwa kutegemea na ujuzi wa watu katika maeneo yao, pia na kupima mwinuko, na mfano wa mitaro itakavyokuwa na vingine.

Kufunza wanafunzi mia tatu katika kutengeneza ramani za kijamii ni changamoto kubwa na fursa! Kupanga kundi kubwa ni kazi/zoezi gumu. Lazima tuhakikishe wanafunzi wanapata ujuzi wenye tija, wanatengeneza taarifa zenye ubora wa hali ya juu, na kufanya kazi kwa ufasaha na wanajamii wanaowazunguka. Kwa bahati nzuri tuna timu inayojumuisha wanafunzi kumi wa zamani katika mradi uliopita wa Ramani Huria ambao wamehitimu na kuwa viongozi; watakuwa nguzo katika kuongoza wanafunzi wapya katika kujifunza njia za kutengeneza ramani.

Wanafunzi wakijifunza kuhusu Ramani Huria na wajibu wao katika mradi.

Kama kawaida, taarifa zinazokusanywa na Ramani Huria ni mali ya watu wa Dar es salaam. Ni taarifa huru, inayopatikana kwa yeyote katika jukwaaa la OpenStreetMap. Sio tu kuwa zinatumika katika mpango wa kupunguza mafuriko, uboreshaji huduma za afya, mitaro, na miundombinu mingine bali watu watazitumia katika njia za bure, ramani za bila mtandao kwenye simu zao za kidigitali na biashara ndogondogo zinaweza kutumia taarifa hizi kuboresha huduma kwa wateja. Ramani zenye ubora wa hali ya juu, zinazopatikana bure na kuwa na taarifa za mitaa zinasaidia karibia kila mmoja,na hasa pale zinapomilikiwa na watu wenyewe!

Kama upo Dar es salaam wiki chache zijazo, tegemea kuona timu yetu jiji zima la dar es salaam wakikusanya taarifa muhimu zitakazofanya jiji liwe bora, lenye nguvu, na sehemu makini. Na pia jaribu kutupia jicho kwenye ramani!

Leave a Reply