Katika heshima ya Siku ya UKIMWI Duniani 2017, Ramani Huria na Tanzania Data Lab (dLab) waliandaa tukio kuongeza ufumbuzi kwa njia ya uwazi, uwajibikaji na ushirikiano. Lengo ilikuwa watu kujifunza jinsi ramani inavoweza kuongeza uhuru na upatikanaji wa habari kwa umma juu ya VVU / UKIMWI katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania. Tuliamua kutengeneza ramani ya Geita wilaya iliyopo katika ukanda wa ziwa Victoria ambapo wilaya hii ni moja ya wilaya zinazongoza kwa ukatili wa kijinsia kutokana ukatili huu watu wamepata ulemavu wa moja kwa moja uliosababishwa na ukatili huo. Ni wazi kuwa maeneo ambayo yana ukatili wa kijinsia pia huwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya VVU / UKIMWI.

 Utengenezaji wa ramani ukiendelea

Katika tukio hilo, watu wa kujitolea walipata utangulizi wa  kwa nini sisi hufanya matukio ya kutengeneza ramani, na jinsi ambavyo tunaleta pamoja waandaaji ramani, wafanyakazi wa kujitolea na jamaa wengine katika uwanja wa kujifunza jinsi ya kuingiza taarifa kwenye OpenStreetMap, kutengeneza ramani za bure/huru na zinazopatikana kwa urahisi kwa ajili ya matumizi ndani ya nchi na ya kimataifa – kwa upande wetu lengo lilikuwa juu ya VVU / UKIMWI.

Washiriki wetu walipata utangulizi juu ya mradi wa Ramani Huria. Walijifunza jinsi ramani husaidia jamii, na jinsi tukio hili linaweza kusaidia kuzalisha taarifa kwa ajili ya watu Geita.

Kabla ya kuanza kuchora ramani, tulihakikisha kwamba kila mtu alikuwa na;

  • Laptop, MacBook, au Desktop.
  • Kipanya (kufanya uchoraji kuwa  rahisi)
  • OSM akaunti (mtu anapaswa kuwa nayo ili kuweza kuingiza taarifa kwenye OSM).
  • Mtandao.

Waliohudhuria walipewa mafunzo ya jinsi OSM inavyofanya kazi, na jinsi ya kuingiza taarifa kwa kutumia JOSM na Id Editor. Baada ya hapo walielekezwa kuhusu  OSM Tasking Manager. Hichi ni chombo cha ramani  kilichoundwa na kujengwa kwa ajili ya watengeneza ramani. Madhumuni ya chombo ni ya kugawanya eneo katika sehemu ndogo ndogo ambazo zinaweza kukamilika kwa urahisi. Chombo hichi  kinaonyesha maeneo ambayo bado yana unahitaji wa kuchora ramani na ambayo yamemalizika ila yana haja ya kuthibitishwa.

Washiriki walianza kutengeneza ramani, wakichora barabara na majengo na baadae kupakia kwenye mtandao.

Kufanya tukio kuwa shirikishi na la kuvutia, tuliofanya michezo kama vile OSM fights. Mchezo huu unakuwezesha kuingiza majina ya watumiaji wawili unaaanza mpambano wa kufurahisha kati majina ya watumiaji wawili kulingana na ‘Jinsi gani mtu kachangia kwenye OSM’. Na mwishowe mshindi ataonekana.

Kutangaza mshindi kila baada ya kila dakika 30 kulileta motisha kwa washiriki kuendelea kuchora ramani kwa kasi. Bila shaka, kila mtu angekuwa na furaha kuona kuwa ni mshindi, hivyo hii ilileta ushindani mkubwa kwa washiriki.

Picha ya pamoja ya washiriki

Tukio lilikuwa  na mafanikio halisi na watu walikuwa na nia ya kujua wakati mwingine wa  kufanya mapathon ili waweze kushiriki tena. Ni fahari yetu kuona jinsi jamii yetu ya watengeneza ramani inakua siku hadi siku.

Leave a Reply