Tarehe 8 hadi 10 Disemba Croud2Map na Ramani Huria walishirikiana kuandaa mkutano wa kwanza wa hali ya ramani uliofanyika Dar es Salaam, Tanzania. Mwanzoni tulitegemea washiriki 150 lakini watu waliofika walizidi makadirio yetu ya mwanzo na kufikia watu 170 kutoka nchi saba:  Malawi, Kenya, Uganda, Rwanda, Zambia, Ujerumani na Tanzania yenyewe. Ilikuwa tukio ambalo liliwaleta pamoja watu wenye taaluma tofauti tofauti kufanya mafunzo, kufahamiana na kushirikiana

Washiriki;

Mafanikio makubwa ya mkutano yalitokana na washiriki kuwa na taaluma tofauti tofauti. Waliohudhuria walikuwa watu kutoka Vyuo vikuu, Vijana watengeneza ramani, wanajamii, watafiti, viongozi wa serikali, idara ya ofisi ya raisi ya Marekani (Programu ya PEPFAR), Mashirika mbalimbali yenye nia ya kutumia ramani kutatua changamoto mbalimbali, wataalam wa compyuta na wafanyakazi wa  HOT. Washiriki hawa wote walitamani sana kujifunza kutoka kwa kila mmoja, kushirikiana na kuelewa jinsi ramani inaweza kuwa sehemu muhimu ya shughuli zao za kila siku.

uwasilishaji.

Timu ya Ramani Huria ilifanya kazi kubwa kuandaa mkutano, na vijana watengeneza ramani kutoka maeneo mbalimbali walikuwa na nia ya kusaidia watu wapya kwenye utengenezaji wa ramani. Ilikuwa ni vizuri kuona mmoja wa vijana kutoka Uganda kufanya mafunzo kwa washiriki kuhusu jinsi ya kutumia JOSM na Id- Editor katika kutengeneza ramani.

Mawasilisho mafupi

Kulikuwa na mfululizo wa mawasilisho ili kuonyesha kwa nini ramani ni muhimu na jinsi zinavyosaidia katika nchi nyingi na miradi. Kulikuwa na uwasilishaji kutoka kwa PEPFAR kuelezea jinsi ramani inavyosaidia kwenye mpango wao wa kuondokana na VVU / UKIMWI. Ramani Huria ilizungumzia kuhusu mradi wao unaoendelea wa ramani kwenye maeneo yenye hatari zaidi ya mafuriko na jinsi ramani zitatumika kwa ajili ya ustahimili na uamuzi. Map Kibera kutoka Kenya aliwasilisha jinsi ramani inavyosaidia katika utoaji wa huduma za kijamii kama usalama, usafi wa mazingira, afya na elimu. Mkurugenzi Mtendaji wa Mkoa wa Kigoma alielezea mpango wa WASH (Maji na Usafi) na jinsi ramani inavyosaidia katika utoaji wa huduma za jamii Kigoma. Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Heidelberg nchini Ujerumani ambao walishiriki katika kutengeneza programu ya Mapswipe pia walitoa maelezo mafupi juu ya jinsi programu hii inatengeneza ramani kwa urahisi.

Uwasilishaji- Ramani Huria

Meneja wa Nchi- HOT Tanzania Mr Ivan Gayton  alitoa maongezi mafupi juu ya mradi wa Mini-Gridi ambao una lengo la kutengeneza ramani za vjiji vinavyoweza kuwekewa umeme kwa kutumia paneli za nguvu za jua. Mradi huu una lengo la kutengeneza ramani za vijiji ambavyo bado havina umeme na kusaidia kutambua sehemu zinazofaa kwa mini-grids za nishati mbadala. Ramani hizi zinaweza kusaidia waendeshaji wa nishati ya jua kufanya haraka ili kutoa umeme mbadala kwa watanzania zaidi. Hii ni nguvu ya nini ramani zinaweza kufanya!

Baada ya mazungumzo hayo kulikuwa na majadiliano kati ya vijana mbalimbali wanaojihusisha na utengenezaji wa ramani, kujadili kuhusu uzoefu wao na nini wafanye kama vijana.

Majadiliano

Mapathon

Mapathon ni tukio linaloratibiwa kwa ajili ya kutengeneza ramani. Watu wanakaribishwa kufanya maboresho ya ramani kwenye eneo na kusaidia kufanya tathmini ya majanga. Mapathon hutumia tovuti ya mtandao kuhifadhi taarifa za ramani, yaani OpenStreetMap. Wakati wa mkutano tuliandaa Mapathon ya kutengeneza ramani ya Wilaya Manyoni- Kazi iliyoundwa kwa ajili ya kutengeneza ramani za ukeketaji wa wanawake. Washiriki walielekezwa kuhusu OSM Tasking Manager  na mafunzo jinsi ya kutumia programu ya  Id Editor  na  JOSM katika utengenezaji wa ramani.

Mapathon

Utangulizi wa QGIS,Map Swipe na Maps.Me

Washiriki walipewa utangulizi juu ya programu ya wazi na bure ambayo hutumiwa kwenye ramani. Watu walikuwa na nia sana ya kujifunza kuhusu QGIS, lakini siku moja ya mafunzo haitoshi kuweza kutengeneza ramani katika QGIS. Ambacho tuliweza kufanya, na ambacho kilikuwa na mafanikio mazuri, ilikuwa ni kuweka programu ya programu ya QGIS kwenye copyuta za washiriki, na kuhakikisha kuwa wote wanajua jinsi ya kuongeza shapefiles na data zinazotumiwa kufanya ramani.

Wakati wa mafunzo ya QGIS kulikuwa na maonyesho mafupi kuhusiana na drone na mpango wa kutengeneza ramani za vijiji vya Tanzania kwa kutumia drones. Dhana ilitolewa vizuri sana na Mr Ivan Gayton ambapo alionyesha haja halisi ya drone kusaidia na maandalizi ya dharura. Kuwa na mzunguko kamili na ufanisi wa majibu unahitaji ramani na eneo lenye vifaa. Ili kujenga ramani hizi unahitaji kukusanya taarifa kutoka kwa jamii kulingana na picha zitakazotumiwa kwa kukusanya taarifa. Ili kuwa na picha unahitaji drone ambayo husaidia kukamilisha mzunguko kwa kutupa picha nzuri ya kukusanya taarifa na hivyo jamii hizi zinaweza kupata msaada bora.

Picha ya Pamoja.

.

Mwishoni mwa Mkutano tulikuwa na mechi ya soka- OSM Tanzania VS Watu wengine, na OSM Tanzania ilishinda mechi.

Ilikuwa tukio la kuvutia sana na la mafanikio. Waandishi wa habari walikuwepo na mkutano wetu pia ulionyeshwa katika moja ya televisheni maarufu nchini Tanzania- International Television network-Tanzania (ITV), kituo cha Kimataifa cha China Global Television Network (CGTN) and Daily news paper

Kwa ujumla, ilikuwa uzoefu mkubwa kwetu kama waandaaji na pia kwa washiriki. Tayari tunatarajia mkutano wa pili wa hali ya ramani Tanzania mwaka 2018!

Leave a Reply