Ramani Huria 2.0 inakusanya taarifa za mitaro kwenye maeneo yaliyo katika hatari ya mafuriko Dar es Salaam. Taarifa hizi zinatumika kutengeneza programu/kielelezo maalum cha mafuriko (flood model) ambayo inahitaji taarifa za mitaro zilizokusanywa kwa usahihi kama urefu, upana, kama mtaro umeziba (kwa majani au vitu vingine), muunganiko na kipenyo (Kwenye kalavati). 

Kutengeneza programu hii, Ramani Huria inafanya kazi na mtaalamu wa hydrolojia huko Deltares– Uholanzi, Hessel Winsemius. Dr. Hessel ni mtaalamu katika uwanja wa hydrolojia, hasa kwenye masuala ya kutengeneza vielelezo vya hatari ya mafuriko kikanda na kimataifa. Wiki hii alikuwa Dar es Salaam, kuangalia suala hili kwa ukaribu zaidi na timu yetu. Moja ya masuala makuu aliyoona ni ugumu ambao timu ilikuwa inapata katika kuhakiki ubora wa taaarifa- ilibidi kutambua makosa, taarifa zilizokosekana na taarifa zinazohitaji marekebishi kwa kienyeji kwenye programu ya QGIS kwa kuangalia sifa za mtaro husika. Hii inachukua mda mrefu na inachosha. Kwa usahihi, hakuna sehemu katika QGIS ambacho inashughulikia mahususi kwenye kuunganishwa kwa mifereji ya maji, hivyo Hessel aliunda programu (Python) lililoitwa Hydro-OSM  kufanya hivyo tu!

Drain Data Check Model

Ili kuhakiki ubora wa taarifa kwa ufanisi zaidi,  Hessel aliunda programu ya Hydro-OSM kwa ajili ya kuangalia ubora na ufanisi wa taarifa. Njia hii inafanya kusafisha taarifa kuwa rahisi zaidi kuliko njia iliyofanyika hapo awali, na hususani inaangalia sifa zinazofaa kwenye mifereji ya mjini. Kwa sehemu zenye makosa au kukosa taariafa, timu itarudi tena kwenye eneo husika kukusanya au kuhakiki taarifa hizo.

Hessel anaamini kuwa kama tukifanikiwa kutengeneza programu hii ya kielelezo cha mafuriko, itakuwa ni mwanzo mzuuri kwa wafanya maamuzi katika jitihada zao za kujenga jiji linalostahimili mafuriko. Pia anatarajia kusaidia wanajamii kutengeneza programu hii ya mafuriko.

Hessel akiangalia ufanyaji kazi wa programu

Lengo la haya yote ni kutumia taarifa za OSM kutengeneza programu ili kulinganishamtiririko wa maji kutoka eneo moja hadi lingine kwenye mtandao kama mitaro na mito nk.

Ili program kufanya kazi, mitaro inatakiwa kuungana zaidi iwezekanavyo. Ingawa baadhi ya mitaro/mifereji Dar es Salaam haijaungana, hessel anaendelea kulifanyia kazi suala hili ili kuona jinsi ya kuweka mitaro ambayo haijaungana kwenye programu.

Taarifa zote hizi zinahitaji muundo kamili wa programu ya ukusanyaji taarifa ambayo Ramani Huria imeshafanikiwa kutengeneza. Zaidi kuhusu programu hiyo ya mifereji ambayo imeundwa unaweza kusoma kwenye blogu iliyopita hapa

Leave a Reply