Ujanibishaji wa sasa unafanyika ili kurasmisha makazi yasiyo rasmi ya Dar es Salaam ambayo sasa inafikia asilimia 70 ya jiji. Kurasimisha makazi kunasaidia kutoa uhalali kwa jamii na kuongeza usalama wa umiliki wa wakazi na haki zao za ardhi. Kujenga makazi pia kunaruhusu mipango zaidi ya kudumu ya mji. Kwa bahati mbaya, mbinu za sasa za ukusanyaji wa taarifa kuelewa mipaka hii imesababisha taarifa zisizo sahihi kutokana na ushiriki mdogo wa wanajamii.

Ili kusaidia kuboresha mbinu za kukusanya taarifa za sasa zinazohitajika kwa ujanibishaji, timu ya HOT  Tanzania imetoa siku tatu za mafunzo na wanafunzi 6 wa elimu ya juu (Masters) wote wakijifunza Mipango na Usimamizi wa Mjini (Msc UPM), na wafanyakazi/wahadhiri 3 wa Chuo hicho. Hadi sasa, mbinu iliyochukuliwa kwenye ramani ya makazi yasiyo rasmi inahusisha matumizi ya picha za drone na satellite ili kutambua mipaka ya makazi. Utaratibu huu sui sahihi, hutumia muda mrefu kwa kuwa  watu wa ndani wamezoea picha za 3D (urefu, upana mna kimo) kila siku za nyumba zao kwenye barabara za mitaani, sio picha ya 2D ya drone (yenye urefu na upana) iliyochukuliwa kutoka juu. Maeneo yenye wakazi wengi pia hufanya kuwa ngumu kutambua nyumba za mtu binafsi na kufafanua mipaka.

Profesa Tumsifu Jonas Nkya (kulia), Daktari(Phd) John Lukenangula (kushoto) wakipakua na kujifunza kutumia Open Data Kit (ODK) kwenye mafunzo kutoka kwa mtaalamu kutoka Ramani Huria Iddy Chazua (Katikati).

Kwa tumaini la kuongeza ushiriki wa jamii na usahihi wa taarifa, timu ya HOT imewafundisha wanafunzi na wafanyakazi kuhusu ramani ya wazi ya jamii. Mafunzo yalihusisha jinsi ya kutumia OpenStreetMap (OSM), JOSM, OpenDataKit (ODK), na OpenMapKit (OMK), (programu za kutengeneza ramani zianzowekwa kwenye simu ili kukusanya taarifa). Kutumia zana hizi, tafiti za kidigitali zinaweza kukusanya taarifa katika ngazi ya mitaa kwa kuzungumza na wenyeji kutambua matumizi ya ardhi, umiliki na matumizi ya majengo, na hali ya kijamii na kiuchumi ya wenyeji. Kuweka sifa ya jengo kwenye OpenMapKit wakati wa kufanya tafiti ya ardhi kutakikisha kuwa matumizi ya ardhi yanaweza kufafanuliwa kwa usahihi zaidi. Kisha taarifa hii inaweza kutumika kupangilia mipaka ya makazi. Njia hii ni ya haraka zaidi na rafiki kwa mazingira zaidi kuliko tafiti za awali za karatasi na hatua ya ziada ya kuingiza taarifa inatolewa kutoka kwenye mchakato. Kwa kuhusisha wanajamii moja kwa moja katika mchakato wa ramani katika muundo ambao wanaweza kuhusishwa, taarifa sahihi zaidi hukusanywa. Wakati ramani ya jamii ikianza, Shina la mtaa (mgawanyiko wa viongozi wa mtaa), Wajumbe, wataongozana na timu ya kukusanya taarifa ili kuzungumza na wenyeji wa eneo kuwahakikishia lengo la mradi.

Mafunzo kwa vitendo kwa kuongozwa na Ivan Gayton, Meneja wa HOT Tanzania.

Ramani zilizotengenezwa kupitia mradi huu zitaweza kupatikana kwa kila mtu mtandaoni kupitia jukwaa la OpenStreetMap. Hii ina maana kwamba kwa mara ya kwanza, wenyeji wa makazi yasiyo rasmi watakuwa kwenye ramani na wanaweza kuingizwa zaidi na kushiriki katika mipango ya baadaye ya mji wao. Ramani zilizochapishwa zitatumika kama kuchora Mipango ya Mji ambayo itajifunza hali zilizopo za jiji na matumizi ya ardhi na kutafakari ambapo rasilimali zinapaswa kupewa au maeneo gani yanahitaji maendeleo. Ramani pia itasaidia kufuatilia mabadiliko katika matumizi ya majengo, kwa sasa, viongozi wa serikali hawana uhakika wa matumizi ya majengo ikiwa mtu anaomba idhini ya kubadilisha kazi ya jengo.

Baadhi ya wanafunzi walioshiriki kwenye mafunzo walikuwa na haya ya kusema:-

“Ramani za kijamii zinaweza kuongeza ushiriki wa jamii na na kutengeneza ramani za  mali zao na kuwashirikisha katika kukusanya taarifs yoyote ambayo ni muhimu kwa shughuli za kuimarisha/kurasmisha makazi” – Luteranya Mapambano mwanafunzi katika taaluma ya mipango miji. 2017/18.

“Ramani ya Jumuiya ni chombo muhimu katika kupunguza muda wa kazi wakati wa kuimarisha/ kurasimisha, kwa kuwa mtu yeyote anaweza kupata taarifa muhimu kama maendeleo na vipengele vingine bila umuhimu wa kwenda kwenye eneo husika” – Jikora, Emmanuel, Mwanafunzi katika taaluma ya mipango miji. 

Leave a Reply