“ Watu hawa hawajawahi kuwekwa kwenye ramani, hakuna mtu aliwahi kuwajali hata kuonyesha nyumba zao zilipo, kwa hiyo nyumba hizi mnazochora leo, ni kwa mara ya kwanza mmmejali kwa kiasi cha kuwaweka hawa watu walio kwenye vijiji vya mbali vya Congo kwenye ramani, Kuwa kwenye ramani ni kutambulika, ni kufahamika, ni kujulikana, ni kuhesabiwa. Ni dunia kujua kuwa una mahitaji, kwamba una thamani, kwamba una haki, na mumefanya haya kwa watu zaidi ya 150000 leo” Ivan Gayton.

Tarehe 9 Juni Ramani Huria iliandaa Mapathon iliyokuwa na lengo la kuchora barabara na majengo kusaidia mashujaa wetu waliopo Congo kupambana na Ebola.

Ni vipi ramani zinaweza kutumika?

Mwaka 2014 ilipotoke mlipuko wa ugonjwa wa Ebola huko Afrika ya magharibi, ambapo watu takribani 12000 walipoteza maiisha, ramani za kidigitali zilionekana kuwa na umuhimu zaidi kusaidia mameneja wanaofanya shuhuli za dharura za kibinadamu

Wakati kuzingatia zana bora na ujuzi wa kukabiliana na mlipuko wa Ebola Afrika Magharibi, mwaka 2014, Madaktari Wasio na Mipaka / (Médecins Sans Frontières (MSF)) walimtuma mtaalam wa masuala ya Kijiografia na ramani (GIS) Guinea kusaidia wauguzi na madaktari wa Guinea na wa kimataifa ambao walikuwa wanapambana na mlipuko wa Ebola. Lengo la kupelekwa hii ni kujua kama GIS inaweza kusaidia katika utatuzi wa tatizi hili. Kitengo cha GIS cha MSF kilimwomba mwezeshaji wa Ebola Timo Luege kuandika utafiti wa kesi unaonyesha faida za afisa wa GIS. Baadhi ya matokeo muhimu yalikuwa;

  • Licha ya kufanya kazi kwenye maeneo ambayo ni magumu kufikika, Mtaalamu huyu aliweza kupata mtandao wa intenet ambao ulimsaidia kuomnba msaada kwa watu walio mbali. Kati ya mambo mengine moja ilikuwa ni kuomba msaada wa watu wanaojitolea kutoka jamii ya OpenStreetMap (OSM) kuchangia chochote kwenya ramani. Hii inaonyesha jinsi makundi ya watu yanaweza kuchangia masuala ya dharura ya kibinadamu kama vile magonjwa ya milipuko.
  •  Afisa huyu wa GIS, pamoja na wafanyakazi wa eneo hilo, waliweza kutoa mchanganuo kutoka kwenye ramani ambazo zilitengenezwa na watu wa mbali. Taarifa zote zilikuwa muhimu (zilizotengenezwa na watu wa pale na wa mbali) bila msaada wa mbaliwa kupata ramani ya marejeo wataalamu hawa wasingeweza kupata ramani ya marejeo ili kuweza kuingiza taarifa walizopata za GIS (mfano maeneo ambayo huduma za afya zilipo) zinazohitajika katika kupambana na Ebola kikamilifu.

Watengeneza ramani wakichora majengo na barabara za huko DRC kwa kutumia- HOT Tasking Manager

Utafiti huu wa kihistoria uliisukuma timu ya Ramani Huria kusaidia mlipuko wa sasa wa Ebola Huko Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Timu ilaamua kufanya Mapathon kutengeneza  ramani za vijiji ambavyo vinaathiriwa na Ebola kwa kuchora majengo na barabara ambapo baadae itasaidia katika kupata ramani ya marajeo kwa wataalamu wa GIS ambao ni nyenzo kubwa katikamashirika ya kibinadamu na ya maendeleo yanayofanya kazi katika maeneo hayo.

Meneja wa HOT Tanzania , Ivan Gayton, alieleza uzoefu wake wa mlipuko wa Ebola huko Sierra Leone ambapo alishuhudia ugonjwa huu hatari huko Africa ya mgharibi akiwa afisa wa MSF (Madakjtari wasio na mipaka). Alieleza washiriki jinsi gani madaktari na maafisa wa afya wanavyofanya kazi na jinsi gani ramani zinaweza kuwasaidia katika kupambana na ebola na hata magonjwa mengine ya milipuko.

Ukuaji wa biashara kwenye vijiji vya Africa, Kasi ya kuenea kwa magonjwa kama Ebola unaweza kuenea kwa kasi kubwa sana. Watu wanaopambana na ebola wanatakiwa kuwatafuta watu walioambukizwa na kuwapa chanjo na kuwatenga na wengine ili ugonjwa usisambae. Kama hakuna ramani, wafanyakazi wa afya watapata shida ya kuwatafuta watu ambao wanaweza kuwa kwenye hatari ya kupata Ebola. Kusaidia katika kutengeneza ramani za mbali inaeza kuwasaidia watu wanaopambana na Ebola kwa kuwatafuta watu wanaoweza kuwa na maambukizi kwenye vijiji vyao na kuweza kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu.

Jumla ya watengeneza ramani 75 na washiriki 94 walifika kwenye mapathon na ndani ya masaa mawili jumla ya nyumba 37,583 ziliwekwa kwenye ramani. Hii n sawa na kueka watu takribani 187,915 kwenye ramani, na kurahisisha katika kutoa misaada ya kibinadamu na kuokoa maisha.

Picha ya pamoja kwenye Mapathon

Tunatumaini taarifa zetu zitatumika katika kutatua tatizo hili na timu ya Ramani Huria ipo radhi kkutoa msaada zaidi wa ramani za mbali kama zitahitajika.

Usefull Links

Leave a Reply