Ramani Huria na Benki ya Dunia inajaribu kutafuta njia nzuri ya kupima mwinuko katika jiji la Dar es Salaam ili kuiunganisha na kielelezo cha mafuriko (flood model) ambacho kinaandaliwa. Kupima mwinuko kunahita mfululizo wa vipimo vigumu.

Mwishoni mwa mwezi wa nne 2018. Wanafunzi watatu wa uhandisi kutoka chuo kikuu cha teknolojia cha Delft  Uholanzi- Huckleberry, Detmar and Martijn- waliwasili Dar es salaam ili kutengeneza vifaa nafuu/rahisi za kupima mwinuko. Watachukua takribani miezi miwili kufanya kazi na timu ya Ramani Huria. Wanaamini Ramani Huria ni timu yenye vijana wanaojituma na wanaweza kufanya Ramani za kijamii kuwa halisi na kuhamasisha utumiaji wa taarifa huru, na wanaelewa umuhimu na ugumu uliopo katika kupasa ramani sahihi hasa katika jiji linalokua kwa kasi kama Dar es salaam.

Lengo la wanafunzi hawa ni kutengeneza madhubuti kifaa kinachopima mwinuko kwa kutumia joto na mgandamizo wa barometa. Wanafanya hivyo kwa kutumia Arduino iliyounganishwa na kifaa cha Bosch BMP280 inside a watertight box. Lengo ni kuondoa usumbufu wowote kwenye sensor na na kupata mwinuko sahihi unaoweza kutumika na kuingizwa kwenye OpenSteetMap.

Hii ni mara yao ya kwanza wanafanya kazi na BMP sensors hivyo ni uzoefu wao wa mara ya kwanza kwa wao kujaribu hizi sensor na kuona jinsi gani hizi sensor zinaweza kukabiliana na hali ya mazingira ya mjini. Kama wakifanikiwa kwenye hili itawezekana kutengeneza kielelezo cha mwinuko kwenye mji mkubwa kama Dar es salaam.

Lengo kuu la Ramani Huria ni kuweza kutengeneza mbinu ya kupima mwinuko wa jiji la Dar es salaam kwa kutumia njia rahisi na pia uwezekano wa kutumia njia hii kwenye majiji mengine ya Africa kama watahitaji.

Tarehe 24 May, majibu ya majaribio ya Arduino yalionyeshwa kwenye wiki ya ubunifu iliyo andaliwa na mfuko wa maendeleo ya kibinadamu. (Humanitarian Development Innovation Fund)

Maonyesho kwenye warsha

Kutokana na majaribio yaiyofanywa hadi sasa sababu nyingi za mazingira kama jua upepo na mvua vimeonekana ni vitu vinavoweza kuangaliwa kwa ukaribu.Hitilafu kamili ya kila sensor sasa inajulikana na inaweza kuangaliwa kwa pointi moja, ambayo lazima itokee kila wakati kipimo kinapochukuliwa. Timu ilielezea kuwa kosa tegemezi linahitaji muda mwingi zaidi kuelewa na kutatuliwa, lakini sasa wanagundua mbinu zaidi ambazo zinafanya kazi na zinaweza kutumika ili kupunguza hitilafu hii. Katika wiki zijazo timu ya Ramani Huria, ikiongozwa na wanafunzi kutoka chuo cha teknologjia Delft, itaanza majaribio kwa kutumia programu ya simu ya Android inayoweza kusoma Arduino na sensor. Programu tayari imejumuisha kifaa cha IIR (infinite impulse response) – (majibu yasiyo ya msukumo usio na kipimo) ambayo inachuja vipimo ili kufanya taarifa iweze kufanya kazi zaidi. Kazi inayofuata itakuwa server inayokusanya taarifa zote za simu hizi kwenyesehemu moja ili ziweze kutumiwa kwa urahisi na zinaweza kuonekana wakati wowotekipimo kilipochukuliwa. Washiriki katika warsha walivutiwa na uwezekano wa vifaa vya bei nafuu, vilivyotengenezwa ndani ya nchi kuongeza viwango vya kutosha katika kuchangia kwenye kupata taarifa bora ya mafuriko na hatua za kuyapunguza.

Leave a Reply