Tarehe 24 May 2018 Ramani Huria ilishiriki kwenye wiki ya ubunifu iliyoandaliwa na Mfuko wa Ubunifu wa maendeleo ya kibinadamu (Human Development Innivation Fund-HDIF) yaliyofanyika kwenye jengo la tumeya sayansi na Teknologia. Lengola sisi kushiriki ilikuwa ni kuonyesha namna gani ubunifu umesaidia mradi wa RAmani Huria Kufanya shughuli za utengenezaji ramani kwa usahihi na kwa kutumia gharama ndogo. Kauli mbiu ya Ramani Huria ni  “local people, local tools, open knowledge” (“wazawa, zana za wazawa na na ujuzi huru”), hii inalenga kwenye kuwapa nguvu wazawa kwa kutumia ubunifu na taarifa zinazohitajika katika kubadili jamii zao kuwa bora zaidi.

Kazi za ubunifu kwenye maonyesho zilikuwa Mbinu za kutengeneza ramani za kijamii na ugunduzi wa ramani za mashina-wajmbe wa nyumba kumi, Utengenezaji wa drone (ndege isiyokuwa na rubani), Utengenezaji wa ramani za mitaro kwa kutumia programu ya ODK, na Kupima mwinuko kwa kutumia Arduino na Barometer.

Ramani za Kijamii

Tangu kuanzishawa kwake mwaka 2015 Ramani Huria imekuwa ikifanya kazi na viongozi wa kata na mitaa kwa kushirikiana na wanafunzi wa vyuo vikuu kukusanya taarifa kwanye maeneo yao, lakini tuligundua kuwa wanajamii hawakuwa huru kujibu maswali ya watu wasiowafahamu pale maswali nyeti yalioulizwa. Awamu hii ya pili ya mradi wa Ramani Huria unafanya kazi na viongozi wa ngazi ya chhini kabisa wajulikanao kama wajumbe- ngazi ya chini kabisa ya uongozi Tanzania. Viongozi hawa wana jukumu la kuongoza sehemu ndogo sana ya jamii na wananjamii wanawafahamu vizuri. RH 2.0 ilianza kwa kuwapa mafunzo wajumbe na wanajamii kutumia simu zao wenyewe na kidigitali kukusanya taarifa kwanye maeneo yao wenyewe.

Mbinu hii iliwezesha ukusanyaji wa taarifa nyiingi sana  ndani ya muda mfupi kulinganisha na njia ya awali ya RH 1.0. Njia hii tunaita “Ubunifu” kwa sababu ni kwa mara ya kwanza ramani ya jiji imetengenezwa kwa taarifa nyingi za kiwango hichi na wanajamii kwa kutumia vifaa/simu zao wenyewe. Kwenye maonyesho wakati tulivyogawanyika kwenye vikundi washiriki walishangaa kuona ramani ya mafuriko iliyotengenezwa kwa kutumia taarifa ambazo zimekusanywa na wanajamii wenyewe – taarifa hizi mara nyingi ni za kuaminika kwa kuwa wanajamii wanayafahamu maeneo yao zaidi ya mtu yeyote.

Picha; Msimamizi wa Ramani za jamii Asha Mustapher,akiiongoza mazungumzo wakati wa maonyesho ya ramani zilizotengenezwa  kwa taarifa zilizokusanywa na wananchi

Matumizi ya OpenDataKit kusanya taariaa za mitaro/ Mifereji

Awali Programu ya ODK ilitengenezwa kukusanya taarifa za zilizo kwenye muundo wa pointi, Ramani Huria ilamua kutumia ODK kusaidia kukusanya taarifa za mitaro kwa kufamya maboresho kidogo kwenye programu hiyo ili iweze kukusanya taarifa zilizo kwenye muundo wa mistari. ODK ni programu maarufu sana kwenye ukusanyaji wa taarifa hasa katima mashirika ya kibinadamu lakini haijawahi kutumika kukusanya taarifa za mitaro na Ramani Huria imefanikisha hili. Soma blogu kuhusu Kujenga zana za wazi kwa ajili ya utengenezaji wa ramani za mitaro hapa

Picha; Timu ya Ramani Huria ikionyesha taarifa za mitaro zilizokusanywa kwa kutumia zana za kawaida. Ramani hizi za mifereji ya maji zitasaidia kupanga mipango ya kuzuia mafuriko.

Kutumia Arduinos na Barometers kupima Mwinuko.

Kupima mwinuko ni ngumu hivyo inahitaji  msingi mzuri wa vifaa ili kuhakikisha kuna usahihi mkubwa iwezekanavyo. Wanafunzi kutoka chuo kikuu cha technolojia cha Delft huko Uholanzi wanafanya kazi katika kujenga vifaa vya kupima mwinuko. Hadi sasa kuna hatua kubwa iliyofikiwa kulewa ni kwa kivipi tunaweza kupima mwinuko kwa usahihi ambao utaongeza usahihi wa kielelezo cha mafuriko cha sasa.

Sababu nyingi za mazingira kama jua upepo na mvua vimeonekana ni vitu vinavoweza kuangaliwa kwa ukaribu.Hitilafu kamili ya kila sensor sasa inajulikana na inaweza kuangaliwa kwa pointi moja, ambayo lazima itokee kila wakati kipimo kinapochukuliwa. Timu ilielezea kuwa kosa tegemezi linahitaji muda mwingi zaidi kuelewa na kutatuliwa, lakini sasa wanagundua mbinu zaidi ambazo zinafanya kazi na zinaweza kutumika ili kupunguza hitilafu hii. Katika wiki zijazo timu ya Ramani Huria, ikiongozwa na wanafunzi kutoka chuo cha teknologjia Delft, itaanza majaribio kwa kutumia programu ya simu ya Android inayoweza kusoma Arduino na sensor. Programu tayari imejumuisha kifaa cha IIR (infinite impulse response) – (majibu yasiyo ya msukumo usio na kipimo) ambayo inachuja vipimo ili kufanya taarifa iweze kufanya kazi zaidi. Kazi inayofuata itakuwa server inayokusanya taarifa zote za simu hizi kwenyesehemu moja ili ziweze kutumiwa kwa urahisi na zinaweza kuonekana wakati wowotekipimo kilipochukuliwa. Washiriki katika warsha walivutiwa na uwezekano wa vifaa vya bei nafuu, vilivyotengenezwa ndani ya nchi kuongeza viwango vya kutosha katika kuchangia kwenye kupata taarifa bora ya mafuriko na hatua za kuyapunguza.

Picha; Wanafunzi kutoka chuo cha Delft Uholanzi na timu ya Ramani Huria wakieleza jinsi Arduino na Barometer zinavyoweza kupima shinikizo la hewa  ili kukokotoa mwinuko

Utengenezaji wa Drone

Ramani Huria imetengeneza drone ya ndani ya nchi na wafanyakazi wetu wa Tanzania kwa lengo la kupiga picha za anga zenye muoonekano mzuri na ubora wa hali ya juu. Picha hii ya anga itakuwa na manufaa katika kutengeneza ramani zitakazotumiwa kupanga mpango wa kupunguza mafuriko.Ubunifu huu utakuwa muhimu kusaidia kuchenga mtazamo wa maendeleo kwa kutumia mbinu ya picha za anga.

Picha; Majadiliano kwenye Warsha na Afisa bunifu wa timu ya HOT Tanzania Bornlove O. Ntikha, akielezea jinsi ya kutengeneza drone na matumizi yake kwenye masuala ya mafuriko

Kubadili mtazamo kupitia ubunifu

Lengo kuu la Ramani Huria kwenye maoonyesho haya ilikuwa kuonyesha umma vafaa vya kawaida (local devices) na mbinu za ubunifu, Njia za kibunifu zinazotumiwa na wazawa kwa kutumia ujuzi wa wazawa vina uwezo wa kuongeza ushiriki wa raia katika kuleta matokeo chanya kwenye jamiii zao, kama Ramani Huria ilivyoweza kukusanya taarifa sahihi za mafuriko kusaidia wananchi. Tunatoa wito kwa wadau mbalimbali wa maendeleo kuona fursa inayotokana na taarifa za kijamii zinazokusanywa kwa kutumia njia kama hizi ili waweze kupunguza gharama za uendeshaji wa miradi na kuongeza tija kwa kukusanya taarifa za mwanzo kutoka kwa wanajamii wenyewe.

Leave a Reply