Mradi wa Ramani Huria n moja kati ya miradi mikubwa ya kijamii inayotekelezwajijini Dar es Salaam. Matumizi makubwa ya taarifa za ramani  zinazokusanywa ni kuongeza ufahamu juu ya majanga ya mafuriko, mazingira ya kupata mafuriko na uwezekano, vipengele vyote vitatu vya mfumo wa hatari. Ramani ya aina hiii, vipimo na hali ya mtandao wa mifereji ya maji ni sehemu muhimu na ina uwezo wa kuanzisha mifano ya vielelezo vya mafuriko ya kina ambayo inaweza kutumika kuiga mfumo wa mafuriko katika uwezo usiokuwa wa kawaida. Mwanzoni tulieleza kuhusu hali ya ramani za mitaro kwenye mradi wa  Ramani Huria 1.0. Sasa ramani ya miraro inachorwa tena kutumia mbinu za kina na umakini kwenye uunganaji wa mifereji. Kata 20 za mwanzo zimeshakamilika na blogu hiii inaonyesha ni wapi tumefikia hadi sasa.

*Imeandikwa na: Hessel Winsemius, Hawa Adinani, Amelia Hunt, Ivan Gayton, Iddy Chazua, Amedeus Kimaro, Paul Uithol*

Mafuriko karibu na daraja la Jangwani Dar es Salaam tarehe 15 Aprili 2018

Timu ya Ramani Huria iliyobobea imekuwa ikikusanya taarifa za  ramani za mitaro, kuzisafisha na kuangalia ubora wa taarifa a sasantuna taarifa sahihi za mitaro katika kata zifuatazo; Mikocheni, Msasani, Kinondoni, Mwananyamala, Sinza, Kijitonyama, Hanansifu, Ndugumbi, Makumbusho, Mzimuni, Tandale, Manzese, Buguruni, Vingunguti, Magomeni, Kigogo, Mchikichini, Ilala, Mkurumula and Mburahati. Sasa tunaonyesha matokeo kwa kutumia ramani za muingiliano, na kurejea nyuma vipi tumefanya kazi hii. 

Mpangilio wa QGIS wa taariifa yote iliyokusanywa ya mifereji ya maji Juni 2018

Ni kiasi gani tupo sahihi kwenye ukusanyaji wa taarifa

Ramani ya mwingiliano inayoonyesha taarifa na usahihi wake

Kwenye ramani ya mwingiliano iliyo onyeshwa hapo juu, maendeleo ya kazi yanaweza kuonekana. Ramani inaonyesha taarifa zote za mistari zilizokusanywa hadi sasa ambazo kwa njia yoyote zinahusiana na mifereji. Kwa kila mfereji taarifa mbalimbali lazima ziikusanywe,  kufuata mfano wa taarifa iliyotengenezwa (pre-defined data model). Hii inaonyesha kuwa kwa kila mfereji wenye sura maalum taarifa sahihi zinakusanywa. Mfano wa data ya mifereji ya maji (drainage data model). uliwekwa kwa kuzingatia usahihi iwezekanavyo kwa njia hii.Tunasema zaidi juu ya hii hapa chini;

Mwonekano wa mwanzo wa ramani hii unaonyesha ubora wa sifa ya “aina ya mtaro” ambapo sifa hii ya aina ya mtaro lazima uonyeshwe kwenye fereji wowote. Rangi kwenye ramani inayo onyesha kijani inamaanisha taarifa zote zipo kamili, njano inaonyesha taarifa imekusanywa lakini haijafuata uutaratibu uliowekwa, orage ni ambapo taarifa zisizo  sahhihi zimekusanywa (mfano maneno badala ya namba) na nyekundu hakuna taarifa iliiyowekwa.

Kwa ufupi, tunaangalia ukusanyaji wa taarifa zenye ubora. Ili kuhakikisha kazi imekamilika tumetengeneza programu ya kuangalia ni vipi taarifa zinakusanywa kwenye ubora.  Utengenezaji wa programu hii ni wa huru kabisa na unaweza kupata maelezo yake hapa https://github.com/openearth/hydro-osm. Timu ya Ramani Huria kwa sasa inatumia programu hii kila siku ili uangalia ubora wa taarifa kwenye taarifa zinazokusanywa sasa. 

Je mistari myeusi inamaanisha nini?

Tangu mara yetu ya mwisho kuangalia taarifa, vitu vingi vimeongezwa kwenye ukaaguzi wetu wa taarifa wa kila siku. Sasa tunaweza kufanya kitu kinaitwa “conditional data models”. Kwamba baadhi ya vitu vinaweza kukusanywa kama kana vipengele vinavyohusika.  Kwa mfano kama aina ya mtaro ni kalavati, pia onyesha muundo wa kalavati ulivyo (kama ni boksi, pembe nne au duara). Na kama kuna mfereji wa duara (kama unavoonekana kwenye picha hapo chini), tena kupima kipenyo, na kama mtaro utakuuwa wa mraba tutapima upana  na urefu. Timu ya kutengeneza ramani hizi imeandaa data model, ya kina sana, kwa ajili ya mitaro  na vitu vingine jijini ambao unafata mfumo huu.

Mfano wa Kalavati, mfano dhahiri wa mtaro wa duara, ambao unahitaji kupima mwinuko kwenye mtaa/barabara jirani, kipenyo, malighafi zilizojengea na kama umeziba au laaa.

Dar es Salaam/Ramani Huria – OpenStreetMap Wiki

Data collected as part of Ramani Huria conforms to a model. The Data Model specifies what types of attributes are…wiki.openstreetmap.org

Umuhimu wa kukusanya taarifa sahihi na zinazohitajika ni kubwa sana. Vipimo ni muhimu kuelewa ni kiasi gani maji yanaweza kusafirishwa kutoka eneo moja hadi jingine. Hali ya matengenezo ni muhimu kuelewa ni kiasi gani kizuizi kinaweza kutarajiwa ndani ya mfereji wa maji na inaweza kuleta uwezekano wa kutumika kutengeneza kielelezo cha athari za hali ya mifereji ya maji iliyo duni ikilinganishwa na hali ya mifereji ya maji iliyo bora.

Ni kivipi tunakusanya vipengele hivi.

Kuwezesha timu inayofanya kazi kuweza kukusanya taarifa hizi, tunatumia programu ya  OpenDataKit (ODK). Hii inaweza kumuongoza kupitia maswali mbalimbali ka akili sana kutumia simu ya mkononi (Smartphone). ODK inaweza kufanya kazi bila mtandao na kuhifadhi taarifa kwa muda kwenye simu. Mtandao ukiwepo taarifa zote zilizokusanywa zinaweza kutumwa kwenye mtandao. ODK inaweza kuuliza maswali. Kwa mfano unachukua taarifa gani “unakusanya taariifa gani” ambapo unaweza ukajibu ni Jengo, mtaa, mtaro, na vingine. Baada ya hapo kama mkusanya taarifa atasema “mtaro” itauliza “ni mtaro wa aina gani” na kulingana na aina ya mtaro itakuuliza  maswali mengine kama muundo na mwelekeo. Kwa njia hii mfumo wa ukusanyaji taariifa unaweza kufuatwa kwa usahihi. Kwa maelezo zaidi kuhusu utengenezaji wa ramani za miitaro, tafadhali rejea blogu yetu hapa kuhusu utengenezaji wa zana za wazi za kukuusanya taarifa za mitaro.

Ukurasa wa dodoso la programu ya ODK

Ni kivipi taarifa za mitaro zimeungana

Ramani ya kwanza ya mwingiliano inaonyesha muundo maalum wa ukusanyajji wa taaarifa uulifuatwa. Hii ni moja ya kitu muhimu sana kwenye utengenezaji wa ramani za mifereji.  Kipengele kingine ni muunganiko wa mifereji. Mitaro ya mijini ambayo ipo sahihi, ungetegemea kuona mifereji yote imeungana na kutiririsha maji yake kwenye mito au baharini.  Kwenye blogu yetu ya kwanza kuhusu swala hili, tuliona kuwa mitaro mingi haiku ungana, lakini tuliona kuwa hiii inawezekana na ukuusanyaji wa taarifa au ndio hali halisi ya mitaro huko mitaani. Hivyo timu yetu ilihakiki kwa kina sehemu ambayo mtaro unaanza na unapoishia. Timu yetu ya kuangalia ubora wa taarifa inajaribu kuona kama mtaro umeungana angalau pointi moja ya mwanzoni na mwishoni wa mtaro. Pointi ya mwisho inaweza kuwa mtaro hauna mwekekeo, kuelekea kwenye mfereji mkubwa wa maji au maji kuelekea kwenye kata jirani kama bado haijatengenezewa ramani. Hpo chiniutaona matokeo ya taarifa zilizokusanya kwenye kata 20 hadi sasa. Karibu mitaro yote inaonekana ya kijani ikimaanisha kuwa taarifa nying za mitaro tayari zimeshakusanywa, (nyekundu inaonyesha hakuna muingiliano na inatakiwa kuangaliwa tena). Ramani pia inaonyesha mwanzo wa mtaro na mwisho kwa nukta za rangi. Nukta za zambarau zinaonyyesha mitaro ambayo inaiishia kokote. Tunaona kuwa maeneo kama haya ni hatarishi, hasa kama kuna mitaro mikubwa inayoelekea maeneo haya.

Hitimisho: RAmani Huria ipo nian kutengeneza ramani kamili na sahihi ya mitaro jijini Dar  es Salaam. Matarajio yetu ni kwamba tunaweza kuanza kujenga kielelezo sahihi na cha kina cha mifereji ya maji ili kuelewa mafuriko, athari zake, na hali ya miundombinu midogo, matengenezo, na taka hatari zinazoweza kusababisha mafuriko. Kipengele kilichokosekana ni . Hatua muhimu taarifa za mwinuuko kutoka usawa wa bahari. Hatua za kupima mwinuko zinaendelea ndani ya Ramani Huria. Tafadhali angalia blogu hii kwa habari zaidi.

Ramani ya muingiliano iinayoonyesha muunganiko wa mifereji mwanzo na mwisho wa mtaro

Leave a Reply