Mkutano ulifanyika kwenye mitaa miwili ya kata kigogo kama majaribio ili kuona ni jinsi gani taarifa za wanajamii zinaweza kuutumika kutengeneza mpango huu.

Picha; Mkutano na Wana jamii.

Tarehe 26 mwezi wa tatu 2018, Timu ya HOT Tanzania ilifanya mikutano ya majaribio kwenye mitaa ya Mbuyuni na Kigogo kati. Lengo kubwa la mkutano ilikuwa kuhamasisha majadiliano na wadau mbalimbali kama Mtendaji wa mtaa, Mwenyekiti wa mtaa Wajume, Asasi zisizo za kiserikali na mashirika ya kijamii kama Tegemeo. (Tegemeo ni shirika linalotoa elimu kwa jamii kwenye mambo ya elimu ya mazingira na kusaidia yatima- Inafanya kazi nchi nzima.

Kwenye mkutano huu, Wanajamii walionyesha maeneolvitu ambavyo wanaona vina thamani sana kwenye mitaa yao. Taarifa hizi zitawezesha Ramani Huria kutengeneza mpango wa kupambana na mafuriko. Ramani hizi zitakuwa ni zao lililotokana na taarifa zilizokusanywa wakati wa mkutano na kupangiliwa kwa kutumia programu ya huru kama QGIS.

Picha- Viongozi wa mtaa wanasoma ramani na kuonyesha makazi yao.

Ninafurahi kuwa sehemu ya zoezi, Kujua nini kinaendelea kwenye mtaa wangu, kushiriki kwenye kutambua maeneo salama na yasiyo salama kwa kutumia ramani ni mwanzo mruri ili kutengeneeza mpango wa kupambana na mafuriko” Mazoea Ling’omba- Mjumbe, Mtaa wa Kigogo Kati.

Mkutano ulihudhuriwa na washiriki 43 kutoka mitaa miwili, kwa mikutano shirikishi iliyo huisha makundi ya watu wanne hadi watano. Zoezi lilianza kwa kuwaelekeza washiriki jinsi ya kusoma ramani, kuonyesha maeneo muhimu na kuonyesha makazi yao. Mwisho wa majadiliano washiriki waliweza kuonyesha nyumba zao na kuongeza majina ya mitaa ambapo kulikuwa hakuna taarifa au hazikuwa sahihi.

Picha; Ramani zinaboreshwa kwa kuongeza taarifa zilizo kosekana, maeneo hatarishi yana onyeshwa kwa vitu muhimu kwenya mtaa..

Najivunia kuwa sehemu ya mchakato huu- Nimepewa  mafunzo ya jinsi ya kusoma ramani, na kuweka vitu muhimu kwenye ramani kuboresha taarifa kwa ajili ya kupambana na mafuuriko” Miraji Simba- Mratibu Red Cross.

Somo muhimu lililo jifunzwa kutoka kwenye warsha hii ni kuwa wanajamii ndio watu muhimu katika kutengeneza mpango huu. Wao wanaweza kutoa historia na mwenendo wa mafuriko na kuonyesha maeneo yaliyo kwenye hatari ya kupata mafuriko ( Kwa mfano mhandisi angeweza kujua ni wapi kuna mafuriko kwa kutumia mahesabu, lakini hawezi kutoa wigo historia na athari halisi za mafuriko)- Taarifa walizotoa wanajamii zinaonyesha mwonekano halisi na mwenendo wa mafuriko na kutoa uelewa zaidi wa jinsi mafuriko yalivo badilika kulingana muda.

Wana jamii na viongozi wa kata walijihakikishia na walikuwa na furaha kuhusu mradi huu pale waliposikia kuwa mpango huu wa kupambana na mafuriko hauhusishi kuwahamisha kwenye makazi yao bali kutengeneza mpango mzuri wa jinsi ya kupunguza mafuriko na na mateso yatokanayo na athari za mafuuriko.

Mwanzoni mimi na jirani zangu tulipta wasiwasi kuwa nyumba zetu zitabomolewa, lakini sasa tuna amani kwa  kuwa mradi umeelezwa vizuri kwetu. Nitaenda kuwaelezea “watu wangu” kwenye shina ili kuwahakikishia kuwa mradi huu ni kwa ajili ya mpango wa kupambana na mafuriko na si kuvunja nyumba”Mjumbe-(jina limehifadhiwa).

Kwenye mitaa hii miwili, matatizo yote yaliyo onyeshwa na wana jamii yanafanana kwa sababu Kata nzima ya kigogo ipo kati ya mito miwili mikubwa- mto  Msimbazi na Kibangu ambayo ni mito “maarufu” inayosababisha mafuriko. Ni wazi kuwa mpango huu wa kuzuia mafuriko unalenga kwenye kuweka mapendekezo ya wana jamii ya vitu vya muhimu ambavyo vipo kwenye hatari ya kupata mafuriko na historia ya maeneo yanayopata mafuriko- Mpango ulioboreshwa wa kupunguza athari za mafuriko unaweza kutengenezwa.

Leave a Reply