Baada ya mchakato wa kutambua maeneo yaliyo kwenye hatari kwenye mitaa 228 ya jiji la Dar es Salaam, Mradi wa Ramani Huria unaenda mbali zaidi na kutengeneza ramani za maeneo ya chini kabisa ya utawala yaliyopo Tanzania (shina). tunafanya hivi kwa kushirikiana na mradi wa Data Zetu  kusaidia katika kufanya maamuzi. Kujua anwani za watu wanapoishi ni ngumu sana kwenye mji ambao haujapangwa. Hivyo kutengeneza ramani hizi kutasaidia kutatua matatizo mengi ya ramani kwa mara ya kwanza. Suala hili ni la muhimu sana na litatumika katika maamuzi kuanzia watu binafsi hadi ngazi ya serikali.

Dar es salaam imegawanyika katika manispaa tano, kata 92 na takribani mitaa 452. Ndani ya mtaa kuna mgawanyiko mwingine unaoitwa shina. Mashina pia hufahamika kama nyumba kumi, kwa kuwa mwanzoni mashina yalikuwa na nyumba kumii tu. Lakini kwa sasa kutokana na ongezeko la watu mijini mashina haya yana nyumba kuanzia 30 hadi 200. Kila shina huongozwa na mjumbe au balozi kwa vijijini.

Shina mwanzoni yalikuwa kisiasa,kulingana na mwongozo wa chama fulani. Hata hivyo wajumbe kwa sasawana kazi nyingi tofauti na za chama, kwanza ndio watu wa kwanza wanaounganisha wananchi na serikali. Japo suala la kisiasa katika shina halijapotea, ila tunaona wanaendelea kukubalika na wanajamii ana viongozi wa vyama vyote na matumizi ya mipaka hii ya shina kutengenezewa ramani na kufahamika kwa kila mmja.

Ramani Huria na Data zetu inalenga kutengeneza ramani hizi kwenye mitaa 84 ya Dar es salaam.  Tangu tarehe 13 septemba hadi sasa data za mashina 106 zimekusanywa na kuchakatwa kwa ajili ya utengenezaji wa ramani.

Msimamizi wa utengenezaji wa ramani akitoa mafunzo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu jinsi ya kukusanya mipaka na kuonyesha ramani ya mashina iliyokwisha japishwa; Picha- Ramani Huria.

Mbinu za utengenezaji wa Ramani hizi.

  • Mwanafunzi atahitaji simu ya mkononi (Android) iliyowekwa programu ya ODK yenye marekebisho ambayo ina uwezo wa kuchukua taarifa za mistari kwa urahisi
  • Mjumbe, ambaye ni kiongozi wa shina atafanya kazi na mwanafunzi (aliyepata mafunzo) ili kupata mipaka ya shina- wakati huohuo mwanafunzi huyo atamueleza mjumbe juu ya matuizi mbalimbali ya ramani itakayo tengenezwa ili kuongeza ari ya usiriki. Mwanafunzi na mjumbe watazunguka katika mpaka wa shina na kujaza taarifa zote zinazotakiwa kama namba ya shina, jina la mjumbe nk.
  • Baada ya hatua hii, mjumbe pamoja na mwanafunzi watatumia picha ya anga iliyochapishwa ili kuhakikisha taarifa ya mipaka waliyokusanya kama ipo sahihi.
  • Mwanafunzi atatuma fomu/dodoso kwenye seva kwa ajili ya michakato mingine.
  • Taarifa hizo zitapakuliwa (download) kutoka kwenye seva ambazo zitafanyiwa kazi kwa kutumia programu ya QGIS, na kuchambuliwa ili kutengeneza ramani hizo za shina

Mwanafunzi akiwa na kiongozi wa shina wakihakiki mipaka iliyochukuliwa kwa kulinganisha picha ya anga na mppaka uliochorwa kwenye

programu ya ODK; Picha Ramani Huria.

Ufahamu Wa Jamii.

Wanajamii walikuwa na mawazo tofauti tofauti kuhusu mchakato huu na wana matarajio makubwa kuwa data hizi zitatumika kwa ajili ya jamii husika, na hili ndilo lengo. Mwenywkiti wa mtaa wa Liwiti alikuwa na haya ya kusema:

“Ramani za mashina zitasaidia kutatua matatizo mbalimbali kwa kuwa watu watafahamu vizuri mipaka yao. Nina furaha kubwa kufanya kazi na shirika hili na ni matumaini yangu wawakilishi wangu amewapa ushirikiano mkubwa, na wamefurahi kufanya kazi nanyie” Abdallah M. Simbili, mwenyekiti wa mtaa- Liwiti

Mjumbe wa mtaa wa msimbazi- Kata ya Tabata akimuonyesha mwanafunzi mpaka wa shina lake wakati wa ukusanyaji taarifa. Picha: Ramani Huria.

Matumizi ya Ramani Hizi.

  • Itawasaidia watendaji wa mitaa kuelewa vizuri maeneo wanayo ongoza.
  • Kipindi cha dharura (kama moto au mafuriko), ramani hizi zinaweza kutuikaa kutoa misaada ya haraka kwa kuwa eneo halisi la tukio linafahamika.
  • Kwenye hospital, kujua watu wanapotoka kwa kujua namba za mashina katika programu ya usajili kuweza kujua ueneaji wa magonjwa kama kipindupindu na utapiamlo kwa watoto.
  • Kusaidia jamii kujua wawakilishi wao katika jamii kwa kuwa migogoro mingi hutatuliwa na viongozi hawa.

Kufahamu maeneo ya watoto wenye utapia mlo na kusaidia kwenye harakati

Utapiamlo bado ni mojawapo ya changamoto kubwa za maendeleo ya binadamu Tanzania. Licha ya kuonekana/kusadikika viwango vya “chini” na vya “kukubalika” vya utapiamlo mkubwa, mzigo wa watoto wasio na chakula ni mkubwa Afrika Mashariki. Inakadiriwa watoto 450,000 nchini Tanzania wamepungukiwa na hawana nguvu, wakati zaidi ya watoto 100,000 huteseka kutokana na aina kali zaidi ya utapiamlo mkubwa.

Pamoja na mzigo mkubwa wa lishe Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, sio tu maisha ya mtu binafsi nchini Tanzania ambayo yanatishiwa, lakini pia maendeleo ya kiuchumi ya kizazi kijacho yanahusika. Watu – wote wazima na watoto – ambao wana uzoefu wenye uzoefu tofauti tofauti wa janga la utapiamlo wajitahidi kutumia fursa, kwa mfano, elimu na ajira ambayo itawawezesha kuboresha maisha yao. Kuelewa athari mbaya zinazohusiana upungufu wa chakula, hususani miongoni mwa watoto, ni muhimu sana na hatua zinazofaa zichukuliwe na watendaji ambao wana uwezo wa kufanya hivyo ili kupunguza madhara hayo.

Eneo la mfano; Hospitali ya Rufaa- Amana Dar es Salaam, Tanzania

Kupitia mradi wa takwimu za Data Zetu, timu yetu imeweza kutumia data ya mipaka ya shina iliyokusanywa kwenye mitaa36 ili kuunga mkono Hospitali ya Amana – moja kato ya hospitali nne za rufaa Dar es Salaam zinazohudumia watu kati ya 800 na 1200 kila siku – katika kuboresha njia zao za kukusanya data ya eneo la mgonjwa na kuimarisha ufuatiliaji wa taarifa za mgonjwa anapotoka. Daktari mmoja wa watoto katika Hospitali ya Amana, Dk. Omari Mahiza, ana hamu kubwa ya kutekeleza mfumo ambao utamwezesha kurekodi na kufuatilia maeneo wanayotoka watoto wenye utapiamlo anaowatibu. Kwa kujua zaidi ambapo wagonjwa wake wanatoka, anaweza kuchunguza kwa nini na sababu za utapiamlo wa watoto kutoka kwenye jamii moja hadi nyingine na, kwa upande mwingine, kujua kwa undani sababu zinazosababisha hali hii kutoka kaya moja hadi nyingine.

Kwa miezi michache iliyopita, timu ya Data Zetu imekuwa ikifanya kazi na kampuni ya IT ambayo imejenga mfumo wa kurekodi wagonjwa kwa njia ya kielektroniki katika Hospitali ya Amana ili kuingiza data ya shina na alama muhimu zinazotambulisha eneo (landmarks) kwenye mfumo huo. Sehemu mpya itakayoongezwa katika programu hiyo ya usajili wa kielektriniki utawawezesha wafanyakazi kurekodi data sahihi ya eneo la wagonjwa ambao wamefika hospitalini na kumsaidia Dk. Mahiza na wenzake kuwa na uwezo wa kubainisha anwani ya wagonjwa wao kwa urahisi. Ikiwa lengo ni kuchunguza matukio maalum ya utapiamlo na tabia zinazosababisha hali hii au kupata chanzo cha kuzuka kwa magonjwa ya msimu, kama vile kipindupindu, ramani za shina zitawezesha hili lifanyike kwa ufanisi zaidi katika jamii husika.

Hatua inayofuata kwa Hospitali ya Amana ni kutoa mafunzo na kujenga uwezo kwa wafanyakazi wa ndani, kama wahudumu wa usajili na wauguzi, kuhusu umuhimu na thamani ya kurekodi data ya eneo  anapotoka mgonjwa wakati wa usajili. Ili kuhakikisha kuna uelewa wa kweli na maslahi kwa wafanyakazi wa kurekodi data ya eneo wanapotoka kwa ufanisi zaidi, timu yetu itazingatia kuwezesha majadiliano na kuonyesha matumizi ya ramani kwa kuonyesha mifano dhahiri ya jinsi gani taarifa hizi zinaweza kuimarisha huduma za afya kwa jamii.

Zaidi ya mipango ya afya, ramani pia zinaweza kutumika katika usimamizi wa maafa, kuwezesha mipango ya haraka ya kukabiliana na maafa na kuongeza ustawi katika kupambana na mafuriko kwa jamii. Kwa mfano, kuwa na mipaka ya utawala katika ngazi ya chini zaidi inaweza kuongeza usahihi katika kutambua maeneo yaliyoathirika na kuharakisha usambazaji wa misaada wakati na baada mafuriko. Vivyo hivyo kuwa na ramani za mipaka ya shina inaweza kuwa na manufaa kwa watendaji wa mitaa wakati wa kuongoza na kutekeleza maboresho ya miundombinu.

Leave a Reply