Februari 28, 2017, Ramani huria ilifanya warsha ya pili ya kijamii katika Tanzania Data Lab (dLab). Warsha ilihusisha watendaji wa kata kutoka katika kata 21 zilizotengenezwa ramani kwa kushirikiana na wanajamii wa Dar es salaam, ambapo ramani za kina zilitengenezwa na wanajamii kwa lengo la kutoa uwanja kwa watoaji uamuzi katika mipango dhidi ya mafuriko na athari nyingine zinazozikumba jamii.

Warsha hii ilikua ya kufuatilia katika warsha ya kwanza ambayo ilifanyika Octoba 2016 na ilihusisha watendaji kata 10 kutoka tandale, Ndungumbi, Buguruni, Vingunguti, Magomeni, Hananasifu, Mzimuni, Manzese, Mwananyamala na Kigogo.

Washiriki ambao ni pamoja na watendaji kata 18 kati ya 21 walioalikwa walinufaika na mradi wa ramani ambao ulihusisha Kigogo, Mburahati, Mzimuni, Mwananyamala, Magomeni, Keko, Temeke, Ubungo, Mchikichini, Makurumla, Ndugumbi, Makumbusho, Mabibo, Vingunguti, Buguruni, Ilala, Msasani na Hananasif. Wahudhuriaji wengine ni pamoja na wawakilishi wa Benki ya Dunia na timu ya Ramani Huria ya Dar es salaam.

Katika neno la ufunguzi, msimamizi mkuu wa ramani, Bwana Innocent Maholi alitoa maelezo kwa ufupi ya malengo ya warsha, kipi kinachotegemewa katika warsha na utambulisho wa jumla wa hadhira. Ili kuweka mfano kwa watendaji kata wengine, watendaji kata waliohudhuria warsha ya kwanza walielezea jinsi walivyo nufaika na ramani, msaada ambao ramani imewapa katika kata pamoja na changamoto na somo walilopata ndani ya mchakato. Hii inasaidia kuelezea watendaji wengine ambao walijihusisha na kubadilishana mawazo katika warsha.

Bwana Bernard Gisunte akishirikisha wenzake jinsi ramani zimeweza kusaidia kata ya Makumbusho

Kutokana na asili ya kawaida ya mazingira ambako hizi kata zipo, zinaathirika kwa matatizo yanayofanana; kwa kiasi kikubwa makazi yasiyo rasmi na bila mpangilio, yamejengwa kando ya mito mikubwa na kadhalika. Kwa matumizi ya ramani, kwa kutaja baadhi, wanajamii wanatumia ramani hizi katika:

  • Uhamasishaji wa watu wanaoishi katika maeneo hatarishi kwa mafuriko. Hii ni matokeo ya ramani ya mitaro na mafuriko ambapo waathirika husisitizwa katika ; i) utupaji taka salama kwa mtu binafsi. Hii inapunguza utupaji taka katika mitaro. ii) mara kwa mara usafi wa jumla katika mazingira, kuhakikisha kwamba mitaro haijazwi taka na iii) uboreshaji wa mfumo wa mitaro ya maji kwa kutumia tarifa katika ramani.
  • Ramani zinatumika kushauri wakazi wapya katika kata wanaotafuta viwanja vya kujenga katika maeneo sahihi kwa ujenzi badala ya maeneo ya maji maji pamoja na utoaji wa lesseni za makazi.
  • Ramani zimeweza kuwasaidia watendaji wa kata kwenye kuweka mipango ya miundombinu ya muda mfupi na muda mrefu kuhusu mafuriko, kwa mfano upanuzi na usafishaji wa mitaro.
  • Utambuzi wa mipaka ya kata na kuelewa maeneo ya utawala pamoja na jiografia ya kata kwa watendaji wapya wateule wa kata.
  • Kuonesha maeneo na jinsi ya kuzunguka kwenye kata, mara nyingi kwa wageni, watendaji wapya waliochaguliwa pamoja na jamii kwa ujumla.
  • Ramani zimekuwa zikisaidia wanafunzi wanaochukua masomo ya juu ya chuo kikuu ambao hufanya utafiti na mafunzo kwa vitendo katika kata hizi.

Kwenye kutumia na kuboresha ramani (OSM), watendaji wa kata walishauri kuongezeka kwa mafunzo ya mara kwa mara kwa wanajamii ili kuwanoa zaidi kwenye ujuzi wa kutengeneza ramani na kuwapatia vifaa vya kutosha vya kufanyia kazi kama GPS, simu na kompyuta. Mwishowe, watendaji wa kata waliahidi kuendeleza ushiriki wao kwenye kazi za utengenezaji wa ramani katika maeneo yao ya utawala.

Picha ya pamoja na watendaji wa kata Dar es salaam.