Attendees at the Scale Up Workshop gather outside Nkrumah Hall. PHOTO CREDIT: Ramani Huria

Waliohudhiria katika warsha ya kuongeza nguvu katika utengenezaji wa ramani wakiwa wamejikusanya nje ya jengo la Nkurumah:PICHA KUTOKA: Ramani Huria.

Dar Ramani Huria warsha ya kuongeza nguvu ya utengenezaji wa ramani, ilifanyika ndani ya jengo la Nkrumah, chuo kikuu cha Dar es Salaam, Jumatatu ya tarehe 6 Julai.Zaidi ya miezi mitatu, Mradi wa Ramani Huria, Utengenezaji wa ramani kwa ushirikiano na Jamii ili kujikinga na maafa ya Mafuriko.,ilifanyika katika kazi zilizopita na kupanua utengenezaji wa Ramani katika kata zaidi ndani ya Dar esSalaam.

Uongezaji wa nguvu ya kutengeneza Ramani iliongozwa na grupu la wanafunzi kumi na tano ambao walifundishwa na Humanitarian OpenStreetMap Team(HOT) na walifanya kazi na Jamii kutengenenza Ramani katika kata za Ndugumbi, Tandale na Michikichini.Katika wiki zijazo mradi utahusisha ongezeka la wanfunzi 140 kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) na Chuo Kikuu Ardhi, pia wawakilishi kutoka katika jamii ndani ya kata 10 hadi 14 ambazo zitatengenezewa Ramani, ikiwa ni pamoja na Makumbusho, Makurumla, Msasani na Mabibo. Kata ambazo zitafuta kutengenezewa ramani katika mradi huu ni zile ambazo zina idadi kubwa ya watu ndani ya Dar es Salaam, na inahusisha makazi yasiyo rasmi. Makazi mengi katika kata hizi yanapatikana katika sehemu hatarishi kwa mafuriko, ambapo inasababisha kupata maafa makubwa mafiriko yakitokea.

Mapping of Dar es Salaam to date CREDIT: Ramani Huria

Utengenezaji wa Ramani Dar es Salaam hadi sasa: PICHA KUTOKA :Ramani Huria.

Warsha ya kuongeza nguvu katika utengenezaji wa ramani ilihusisha paneli mbili na ushiriki wa wanafunzi katika warsha, wakiwepo wanafunzi na wawakilishi kutoka katika kata waliohudhiria. Mgeni Rasmi katika tukio  hilo alikuwa Julia Letara, afisa mipango miji kutoka Manispaa ya Kinondoni.

Guest of Honour, Julia Letara PHOTO CREDIT: Ramani Huria

Mgeni Rasmi, Julia Letara, PICHA KUTOKA: Ramani Huria

Tukio lilifunguliwa na  Dr, Mwanukuzi, Mkuu wa idara ya Geographia(UDSM), alieyemwakilisha mkuu wa chuo cha sanaa na sayansi ya jamii(UDSM), na Mgeni rasmi, Mrs Julia Letara, Mkuu wa Maafisa Miji katika manispaa ya kinondoni.

First panel (L-R): M.Iliffe, J.Letara, Dr P. Mwanukuzi, H.Hambati, G.Kateregga PHOTO CREDIT: Ramani Huria

Paneli ya kwanza(L-R): M. Illife, J..Letara, Dr.  P . Mwanukuzi, H . Hambati, G. Kateregga. PICHA KUTOKA :Ramani Huria

Paneli ya kwanza, “inahusika katika kutengeneza ramani za mafuriko”, ilianza kwa kuelezea  “Hali yetu ya Ramani” aliongelea Geofrey Kateregga, Mratibu wa ramani kutoka HOT. Paneli ilihusisha:Julia Letara(mkuu wa mipango miji Manispaa ya kinondoni), Mark Ilife(Mtaalamu wa geospatial kutoka Benki ya dunia); Dr, Mwanukuzi (Mkuu wa Idara ya geographia (UDSM), Dr, Hambati(USM) na Geoffrey Kateregga(Mratibu MKuu wa utengenezaji wa Ramani kutoka HOT). Paneli hii ilitoa maelezo ya Jumla  juu ya mwelekeo na kufanikiwa kwa  mradi wa ‘Utengenezaji wa Ramani za  kujikinga na Mafuriko, na utambulisho wa vifaa vya uchoraji wa ramani vinavyotumika katika uvhoraji wa Ramani.. Mgeni rasmi, Julia Letara, alielezea teknolojia mpya inatoa fursa nyingi, inahusisha kuwapa raia sauti na kusaidia kujua namna ya kupata na kutoa huduma za jamii.

Second panel (L-R): V. Deparday, D.Minja, K.Hamis PHOTO CREDIT: Ramani Huria[

Panel ya pili(L-R): V. Deparday, B. Minja, K . Khamis: PICHA KUTOKA :Ramni Huria.

Paneli ya pili, “Kuunganisha Jamii” ilianza na kwa kuelezea “uzoefu wa  kimataifa wa utengenezaji wa ramani” na Vivien Depardy kutoka  Ktuo cha Kimataifa cha KupunguzaMajanga na Ahueni (GFDRR). Paneli hii ilihusisha Deogratias Minja(Mshauri  wa takwimu za wazi, kutoka Benki ya Dunia);Vivien Deparday(Mtaalamu wa Majanga, kutoka Benki ya Dunia na Kamal Khamis, Mwanajamii kutoka kata ya Ndugumbi. Ilifuata kipindi cha maswali na majibu, kwa kuzingatia utengenezaji wa ramani kwa kushirikiana na Jamii kwa upande wa Dar es Salaam, hasa namna taarifa zinavyokusanywa kwa kutumia uaandaaji wa Ramani hii itatumika katika mipango na kupunguza maafa.

Kufuatia paneli zote mbili, kulikuwa na muda wa chakula cha mchana, ambapo wanafunzi walirudi kwa ajili ya mafunzo ya “namna ya utengenezaji wa ramani”, iliyoongozwa na timu kutoka HOT.

Students in the practical workshop PHOTO CREDIT: Ramani Huria

Wanafunzi wakiwa katika mafunzo ya vitendo katika warsha:PICHA KUTOKA:Ramani Huria

Sehemu  ya kwanza katika warsha ilianza na kuelezea mbinu za uchoraji wa Ramani. Kuongeza kasi katika kazi za miradi, HOT wamenunua ndege ndogo bila rubani(Drones) kutoka senseFLY, ambazo zitasaidia kutoa picha za angani zenye muonekano wa hali ya juu ambazo zitasaidia kutengeneza ramani kwa urahisi na sahihi zaidi. Ilihusihwa katika kufungua warsha  ilikuwa ni maelezo mafupi ya vitendo na maelezo ya jumla kuhusu Ndege ndogo ya juu (Drones), aliongoza Mark Ilife kutoka Benki ya Dunia. Sehemu ya pili ya washa wanafunzi waliruhusu wanafunzi kufanya mazoezi namna ya kutumia mbinu mpya za uchoraji wa Ramani na kuanza kutumia mafunzo waliopewa ya kwanza.

Kufuatia warsha ya kuongeza nguvu katika utengenezaji wa ramani wanafunzi walipewa  mafunzo yaliyokamilika juu ya vifaa  na mbinu za  uchoraji wa ramani(Julai 7-9), kabla ya kuanza kwa utengenezaji wa ramani (julai 13).Vifaa vya mafunzo vilivyotumika vinapatatikana katika tovuti ya  mradi ndani ya Github ndani, ya  https://github.com/hotosm/RamaniHuria.