Rasilimali

 

Mradi wa Ramani Huria umewafunza wanajamii na wanafunzi na kuwafanaya wawe na ujuzi na uwezo wa kuchangia na kutengeneza ramani za Dar es salaam, ambayo imepelekea utengenezaji wa ramani za hali ya juu na zenye ubora.

Mtu yoyote anaweza akabadili au kuongeza taarifa katika OpenStreetMap na linki zifuatazo zitakuongoza katika kukupa mwanzo mzuri wa kuanza.

Ramani Huria mara kwa mara hutoa repoti kuhusu hali ya mradi na jinsi inavyokwenda. Zinapatikanika

Vitu vilivyo kusanywa na Ramani Huria vilikusanywa kutokana na data modo. Hii inaonyesha ni vitu gani vinapashwa kukusanywa. Na ni kitu gani kinapashwa kukusanywa kwa kila aina ya data inayotakiwa. Pia inapatikanika katika Github (pamoja na rasilimali nyingi za Ramani Huria).

Chini ni baadhi ya vifafaa vya mafunzo tulivyovitumia kwenye mradi, ilijumuisha OSM,QGIS na InaSAFE.unaweza kupata mafunzo yetu katika ukurasa wa GitHub.

Warsha ya kuongeza nguvu katika uchoraji wa Ramani

Kufuatia warsha ya kuongeza nguvu katika uchoraji wa ramani ambayo ilifanyika katika ukumbi wa Nkrumah, Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Jumatatu ya tarehe 6, Julai. Ramani Huria iliendesha mafunzo kwa wanafunzi 140 wa vyuo vikuu, kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu Ardhi. Wanafunzi hawa kisha watahusika katika kutengeneza ramani za kata ndani ya Dar es Salaam.

Siku 1, 8 julai 2015
Siku ya pili, tarehe 9 Julai 2015
Siku ya 3, 10 julai 2015

Ramani huria imetoa mafunzo juu ya InaSAFE, program inayotoa uhalisia wa madhara ya majanga asili kwa ajili ya mipango bora, kujiandaa na majibu ya shughuli. Inatoa njia rahisi lakini nzuri kukusanyia taarifa kutoka kwa wanasayansi, viongozi wa serikali na jamii kuangalia kwa kina kuhusu madhara yanayoweza kutokea kwa matukio ya majanga baadaye.

Warsha ya kufunga Ramani Huria ilitoa fursa kuonyesha matokeo ya mradi,njia zilizotumika na mawazo yakinifu kwaajili ya baadae na katika utengenezaje wa ramani baadae kwaajili ya maendeleo ya Tanzania.Siku hizi mbili zilitumika kuwahusisha watengeneza ramani za jamii,watu wa serikali na wataalam kutoka katika maeneo mbalimbali kwenye mjadala wa maendeleo na umuhimu wa njia za kutengeneza ramani za jamii Dar es Salaam.viwasilishi kutoka kwa mijadala,jopo la wadau,maongezi yanapatikana hapa kwaajili ya kumbukumbu yako.

Keynote
Panel 1: Flooding in Dar es Salaam
Panel 2: Learning from Ramani Huria
Panel 3: Maps in an Urban Environment
Lightning Talks: Methods & Processes
Lightning Talks: New Technologies
Forecast-based Financing:
Panel 4: Scaling Ramani Huria