Kufuatia  warsha ya kutengeneza ramani kwa kushirikisha jamii kuzuia mafuriko iliyofanyika jumatatu ya tarehe 6 Julai, 2015 wanafunzi wengi walihamasika kujiunga na mradi wa Ramani Huria, kutumia ramani kusaidia kupunguza madhara ya mafuriko ya kila mwaka. Ramani Huria iliwachukua wanafunzi mia moja na hamsini kwa ajili ya mafunzo ya utengenezaji wa ramani, ilijumuisha wanafunzi wa mwaka wa mwisho wa masomo kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam na chuo kikuu Ardhi.

Example of JOSM in use. PHOTO CREDIT: Ramani Huria

Mfano wa JOSM kwenye matumizi. PICHA: Ramani Huria

Wanafunzi waliochukuliwa kufuatia kushiriki siku tatu za warsha ya mafunzo iliyokuwa imefanyika katika chuo kikuu cha Dar es salaam. Mafunzo yaliyanyika chini ya usimamizi wa wasimamizi kutoka chuo kikuu Ardhi, Ambao walipata mafunzo ya awali ya miezi mitatu pamoja na Ramani Huria. Siku tatu za mafunzo kwa wanafunzi wapya ilijumuisha utangulizi kwa  OpenStreetMap (ramani inayoweza kuhaririwa bure) na vifaa vya kufanyia ramani kama karatasi za kazi (hujumisha matumizi yake na namna ambavyo mtu anaweza kuitengeneza) na vifaa vya GPS (eTrex 30), vinavyotumika kurekodia njia na kufuatilia. Na kwa nyongeza katika mitaala ya kufundishia, mafunzo yalijumuisha mafunzo ya  OSM Tracker (na program ya bure ya simu ya Android ambayo inapatikana kwenye Google Play Store) ambayo inafanya kazi sawa na vifaa vya GPS kwa ajili ya ukusanyaji wa taarifa, lakini ina mwonekano rafiki kwa mtumiaji. Na mwisho mafunzo yalitolewa kwa JOSM ambayo ni program ya bure ya kuhariri kwenye OpenStreetMap. Mbinu na njia mbalimbali zilifundishwa katika kipindi cha mafunzo

Students at scale up training PHOTO CREDIT: Ramani Huria

Wanafunzi wakiwa katika mafunzo PICHA: Ramani Huria

Kwa siku mbili za mafunzo ilikuwa ni nadharia na siku ya tatu na nne ilikuwa ni vitendo. Wanafunzi walitumia maarifa mapya waliyoyapata kwa kutengeneza ramani katika maeneo ya chuo kikuu Dar es salaam.

Kufuatia kipindi cha mafunzo Ramani Huria ikawa imewezesha watumiaji mia moja na hamsini kwenye OpenStreetMap kutoka vyuo vikuu viwili. Wanafunzi hawa watakuwa sehemu ya jamii inayoshiriki kutengeneza ramani katika kata sita za Dar es salaam. Kata hizi zimechaguliwa kutoka kwenye kata kumi na saba ambazo zina mafuriko , nazo ni Mabibo, Mburahati, Makurumla, Makumbusho Msasani and Keko.

Katika hatua ya baadaye, taarifa zinazokusanywa na kuhaririwa kwenye OpenStreetmap zitakuja kutumika kwenye InaSAFE (program ya bure inayotikana kwenye  QGIS) kusaidia mfano wa mafuriko uliotengenezwa na ambao utatupatia taarifa za kusaidia kuruhusu upangaji bora na majibu ya mafuriko kwa ofisi za serikali.

Students at scale up training PHOTO CREDIT: Ramani Huria

Wanafunzi katika mafunzo PICHA: Ramani Huria

Kwa kushiriki katika mafunzo wanafunzi wamepata mbinu ambazo walikuwa hawafundishwi kwenye mitaala ya shule, wamepewa faida katika ajira hapo baadaye. Na kwa nyongeza Ramani Huria inakusudia kuwa na watengeneza ramani hai baada ya kumaliza malengo yake. Njia mojawapo ya kulifanya hili liwe kwa vitendo ni kuwa na sherehe ya kutengeneza ramani kila mwezi. Hii iko wazi kwa washiriki wote wa jamii, na kwa nyongeza, tunawakaribisha wenye shauku na wale wapya kusaidia kuhariri maeneo yanayohitaji kuwa na ramani kwa kutumia HOT Tasking Manager. Kaa tayari kwa ajili ya taarifa mpya yoyote kwa ajili ya sherehe ijayo ya kutengeneza ramani na njia za nyongeza za namna unavyoweza kushiriki kwenye utengenezaji ramani unaoshirikisha jamii!

This article has 2 comments

 1. ABEL BAGONZA

  I have enjoyed to be with you in Vingunguti Ward for almost a week from 11 to date sept, 2015. I have enjoyed to interact to some of you in that piece of work at particularly Mtakuja area, Mississpi and Titanic streets gathering relevant data, and i really learning alot the issue pertaining mapping procedures and collecting data using aerial photography. I could not proceed with u till end because even me i’m doing field work activity to accomplish my studies. I hope to see you if our almighty God wish.
  All the best
  Bagonza, Abel
  MSW st persuing at ISW.

  • sophie.lafayette@hotosm.org

   Thanks Abel for the wonderful comment. We’re really glad you are part of the mapping process and that you’re learning about various mapping tools. We hope that your work with Ramani Huria can help with your studies & that you’ll continue to be part of the mapping community in Tanzania!