Warsha ya Watendaji wa Kata Kungumzia Matumizi ya Ramani Kuzuia Mafuriko

Februari 28, 2017, Ramani huria ilifanya warsha ya pili ya kijamii katika Tanzania Data Lab (dLab). Warsha ilihusisha watendaji wa kata kutoka katika kata 21 zilizotengenezwa ramani kwa kushirikiana na wanajamii wa Dar es salaam, ambapo ramani za kina zilitengenezwa na wanajamii kwa lengo la kutoa uwanja kwa watoaji uamuzi katika mipango dhidi ya mafuriko na athari nyingine zinazozikumba jamii. Warsha hii ilikua ya kufuatilia katika warsha ya kwanza ambayo ilifanyika Octoba 2016 na ilihusisha watendaji kata 10 kutoka tandale, Ndungumbi, Buguruni, Vingunguti, Magomeni, Hananasifu, Mzimuni, Manzese, Mwananyamala na Kigogo. Washiriki ambao ni…Read more

Utafiti wa ramani kama mchakato wa jami

Katika kazi ya Ramani Huria ya utafiti wa ramani, wanajamii wamekuwa ni sehemu ya mchakato. Uwepo wao umeleta mafanikio makubwa na kuwahi kumalizika kwa uandaaji ramani katika kata zao. Kwa nini tunatumia wanajamii? Wanauelewa wa ndani kuhusu eneo lao wanaloishi. Hii inamaanisha, wanajua ndani na nje ya maeneo yanayoandaliwa ramani kutokana na ukweli kwamba wamezaliwa pale au wameishi hapo kwa muda mrefu. Kiuhalisia, wanajamii wameweza kuwaongoza timu ya Ramani Huria kwenye maeneo hatarishi na maeneo mengine muhimu kwa msaada wa picha za anga. Wanehakikisha usalama kwa waandaaji ramani(wanafunzi wa Chuo Kikuu), kutumia uanajamii…Read more

Jinsi ya kutengeneza ramani – ramani tuli kwa kutumia QGIS

Unapotengeneza ramani, aidha unaweza kutengeneza ramani tuli ( ambazo hazibadiliki, kwa mfano kuchapisha nakala za ramani) au ramani zinazobadilika (ambazo zinabadilika kama chanzo kikibadilika. Kama ambavyo OpenStreetMap (OSM) inabadilishwa, na kupatikana kidijitali kwa njia ya mtandao). Ramani zetu zote zinachora taarifa kutoka OpenStreetMap na taarifa zote tunazokusanya zinapelekwa katika jukwaa hili. Kutengeneza ramani za tuli, Ramani Huria inatumia programu ya GIS, QGIS na kutengeneza ramani zinazobadilika mara nyingi hujulikana kama “slip maps”, tunatumia programu ya Mapbox Studio. Katika blogu hii, tutaelezea jinsi ya kutengeneza ramani tuli kwa kutumia QGIS. Kama unavutiwa kutengeneza ramani…Read more

Jinsi ya kutumia: QGIS na InaSAFE

QGIS ni chanzo huria na jukwaa la mfumo wa taarifa za jiografia (GIS). pragramu imeundwa na watu wa kujitolea kutoka kwa programu ya jamii huru na vyanzo huria (FOSS) na ipo vizuri katika msitari na mbinu ya Ramani Huria ya kutumia vifaa vya vyanzo vya wazi wakati wowote iwezekanavyo. QGIS inaendesha programu kama Linux, Unix, Mac OSX, Windows na Androids na inasaidia vector, raster mbalimbali na muundo wa database na jinsi unavyofanya kazi. QGIS pia inasaidia idadi ya programu saidizi ambazo zinaweza kutoa  kwa mtumiaji visaidizi vingi vya ziada. Moja ya hizi programu…Read more

(English) Maps for Saving Lives: a revival of Maptime Tanzania

Mwezi Januari tarehe 28, watu 25 wakiwemo, jamaa ,wanafunzi na wadau walikutana  Tanzania Data Lab (dLab) kwa ajili ya tukio la Maptime lililoandaliwa na Ramani Huria. Tukio lilianza saa nne kamili asubuhi na washiriki waliokuwa na shauku walikaa zaidi ya muda uliopangwa ambao ulikuwa saa saba mchana. Lengo kubwa la mapathon hii lilikuwa ni kutambua/kuonyesha majengo na barabara katika wilaya ya Shinyanga ili kusaidia watu wanaofanya kazi na PEPFAR, mpango wa kuzuia na tiba dhidi ya  Virusi Vya Ukimwi. Eneo hili likitengenezewa ramani, PEPFAR na wadau wake wataweza kuonyesha ni jinsi gani jamii…Read more

Ramani Huria ikifundisha wanafunzi wa secondari katika kambi ya vijana ya STEM

Wiki ya kwanza ya Januari 2017, kundi la wanafunzi 60 wa shule za sekondari walikusanyika katika chuo kikuu Marian, Bagamoyo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo katika Kambi ya Vijana ya sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM) yaliyoandaliwa na Projekt Inspire kwa kushirikiana na Timu ya Ramani Huria. Wanafunzi hawa walitoka mikoa tofauti ya Tanzania (Dar es salaam, Moshi, Arusha, Mbeya na kadhalika), walikua pale kwa ajili ya kutambulishwa GIS na ramani za mtandaoni. Kambi za Vijana za STEM ni mpango wa Projekt Inspire. Mpango huu unasaidia kuboresha ubora wa elimu ya sekondari…Read more

Jinsi ya kukusanya taarifa za maeneo kwa kutumia picha za anga

Ukusanyaji wa taarifa kwa kutumia picha za aanga zenye muonekano maridhawa (wahali ya juu) ni sehemu ya mkakati wa mradi wa Raman Huria. Hii inahusisha wa chora ramani kwenda maeneo yao ya kazi kwa ajili ya ukusanyaji takwimu kwa msaada wa karatasi  zinazozalishwa kutoka picha ya anga (drone mbtiles) ambapo karatasi hiyo ya kazi husaidia katika kutoa mwelekeo na kuonyesha maeneo kwa mkusunyaji taarifa.Pamoja na vifaa kama GPS, Timu ya Ramani Huria iliweza kukusanya taarifa za kata zilizopo katikati ya mji, hizi ni pamoja Kivukoni, Kisutu, Kariakoo, Jangwani, Gerezani, Mchafukoge, Upanga Mashariki na…Read more

Kongamano Ramani Huria

Tarehe 7 na 8 mwezi Novemba ilikua ni mwanzo wa enzi mpya ya Ramani Huria - mradi ambao kwa kipindi cha mwaka uliopita ulileta pamoja muunganiko wa aina mbalimbali ya washirika ikiwa pamoja na Tume ya taifa ya sayansi na teknolojia, Benki ya dunia, chama cha msalaba mwekundu cha Tanzania, Marekani na Denmark,Humantarian OpenstreetMap Team, serikali ya tanzania na wanafunzi wa chuo kikuu ardhi na cha Dar es salaam kutambua uwezo wa data zilizotengenezwa kwa ramani jamii na kuendesha uvumbuzi katika mbinu za kisasa za ramani. Watengeneza ramani za jamii, maofisa wa serikali…Read more

Kusherehekea siku ya GIS Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Katika kusherehekea siku ya GIS (mfumo wa taarifa za kijografia) duniani siku ya tarehe 16 na 17 2016, timu ya ramani huria ilikuwa sehemu ya maadhimisho hayo katika ukumbi wa Nkrumah chuo kikuu cha Dar es salaam. Tukio hili lilipewa jina la ‘’Taarifa zinazohusiana na eneo na teknolojia ya taarifa na mawasiliano katika ufumbuzi wa kibiashara’’. Tukio lilihudhuriwa pia na wadau mbalimbali wa GIS kama iBridge Group of Companies, Kilimanjaro GeoConsultant, Chuo kikuu cha Turku - Finland, Arbonaut - Finland, Human Settlements Action Company (HUSEA), Agroinfo (ICT for Agriculture), VIONCE, Tume ya ardhi…Read more

Watendaji wa kata wakishikishana uzoefu na watengeza ramani jamii

Mhamasishaji Msilikale Msilanga akichukua taarifa kutoka kwe mtendaji wa kata ya Tandale, Athuman Mtono PICHA: World Bank Mnamo Oktoba 27, 2016, Maafisa Watendaji wa Kata (WEOs) kutoka jijini Dar es Salaam walikusanyika ili kujadili faida walizoona na manufaa ya baadaye ya mradi wa wanajamii wa  Ramani Huria. Warsha hiyo  ilitanguliwa na taarifa na kiongozi HOT, Innocent Maholi, juu ya faida ya ramani jamii kwa ajili ya kuzuia mafuriko,majadiliano yaliwahusisha na watendaji wa kata, Osiligi Lossai, na uzoefu wa jamii yake na mafanikio na ramani, na majadiliano ya wazi kati ya maafisa wa kata…Read more