Unapotengeneza ramani, aidha unaweza kutengeneza ramani tuli ( ambazo hazibadiliki, kwa mfano kuchapisha nakala za ramani) au ramani zinazobadilika (ambazo zinabadilika kama chanzo kikibadilika. Kama ambavyo OpenStreetMap (OSM) inabadilishwa, na kupatikana kidijitali kwa njia ya mtandao). Ramani zetu zote zinachora taarifa kutoka OpenStreetMap na taarifa zote tunazokusanya zinapelekwa katika jukwaa hili.

Kutengeneza ramani za tuli, Ramani Huria inatumia programu ya GIS, QGIS na kutengeneza ramani zinazobadilika mara nyingi hujulikana kama “slip maps”, tunatumia programu ya Mapbox Studio. Katika blogu hii, tutaelezea jinsi ya kutengeneza ramani tuli kwa kutumia QGIS. Kama unavutiwa kutengeneza ramani mbadiliko za kidijitali, tafadhali ona/fuata kwenye huu ukurasa wa mtandao; How to: Map creation – dynamic slippy maps with Mapbox Studio.

Tumetanguliza QGIS kwenye kipengele kilichopita, inajumuisha jinsi ya kuweka  programu na kuweka INASAFE plugin, kuhakikisha unaweza kusoma hicho kipengele kwanza na ukiwa umeshaweka programu ya QGIS kwenye kompyuta yako.

Kwa nini tunatumia Qgis kutengeneza ramani tuli?

Ramani Huria imefanya juhudi kutumia programu ambazo chanzo chake kiko wazi na vifaa popote inapowezekana. Si kufanya hivyo tu, hii iko sambamba na maadili ya kutengeneza ramani kijamii na taarifa za wazi, inawezesha wanafunzi wetu na wanajamii watengeneza ramani watakuwa wanapata vifaa na maarifa ya kutengeneza ramani zao wenyewe. Programu ya QGIS chanzo chake ni cha wazi, ni bure kwa mtu yeyote kuipata na kuitumia. Kwa kuongezea, inawezesha InaSAFE plugin(ona hii blogu kwa maelezo zaidi) ambacho ni kifaa muhimu sana cha kuchambua taarifa kwenye kesi za majanga, hususani kwenye kesi ya mafuriko kaitika mkoa wa Dar es salaam.

Kipindi unapoanza na QGIS, zifuatazo ni hatua zitakazokuelekeza jinsi ya kutengeneza ramani kwa kutumia QGIS. Mfano, tutakuwa tunatumia taarifa kutoka mradi wa Ramani Huria na kutengeneza ramani ya ujumla ya kata ya Buguruni- Dar es salaam.

Kutumia QGIS kutengeneza ramani

 1. Chukua/Pakua mradi wa Ramani Huria wa QGIS unapatikana kwenye ukurasa wa GitHub account page (chini ya kipengele cha QGIS, halafu chukua faili la ‘Dar es salaam zip’. Kama kikumbushia cha pembeni, mitindo ya tunayotumia inatokana na mfumo usiobadilika wa OpenStreetMap ijapokuwa inajaribu kuchukuliwa taratibu kuonyesha taarifa za ziada za kina kwenye alama kama vile mitaro, njia za maji, aina za majengo na matumizi ya ardhi.
 2. Zikishachotwa, ‘fungua faili’ la ‘Dar es salaam’ na unapaswa kuona mafaili saba kwenye faili jipya.
 3. Chota ‘shapefiles’ kwa Dar es salaam yote kwa kutumia OSM Export Tool(mwongozo wa hatua kwa hatua kutumia hiki kifaa inaweza kupatikana hapa: How to: HOT’s OSM Export Tool).
 4. Pindi shapefile zikiwa zimeshachotwa, zinakili kwenye folda ya ‘shapefile’ katika folda lililoondolewa la ‘Dar es salaam’.
 5. Fungua QGIS na fungua faili ‘DarEsSalaam.qgs’ katika faili lililoondolewa (unaweza kufungua faili kutoka QGIS au bonyeza mara mbili faili litafungua programu.
 6. Subiria kwa muda wakati programu inapozunguka kwenye ramani ya QGIS. Wakati inamaliza, QGIS itaonekana sawa na muonekano ufuatao;

  Mradi wa Ramani Huria ukiwa katika QGIS

 7. Navigate within the map by using using the left mouse button (or equivalent) to drag the map and zoom in or out by using the mouse wheel (or equivalent). As the shapefiles are large, you may experience some delay when navigating as the map is rendered.

Kutengeneza ramani kwa QGIS

Kwa mfano wetu, tutatengeneza ramani ya ujumla kwa kata ya Buguruni iliyopo Dar es salaam. Kwa kufuata hizi njia, unaweza kutengeneza ramani ya kisasa na yenye maelezo mengi, zinazofanana na zile tunazopeleka kwenye kata ambapo tunafanya shughuli za kuaandaa ramani.

 1. Hakikisha kwenye upande wa kushoto wa QGIS tabaka zifuatazo ziko hai; Mipaka; Barabara na majengo; maelezo ya jumla; na bahari. Hizi tabaka zitajumuishwa kwenye ramani

  Chagua ‘properties’ kwa ‘tabaka la mipaka’ kwenye QGIS

 2. Kwanza tunahitaji kutengeneza mpaka wa kata. Kwa kufanya hivyo, kata ya Buguruni itasimama kama yenyewe, na kata zinazozunguka zitakuwa hafifu- hii itaonyesha wazi kipande kipi cha Dar es salaam kinaleta taarifa. Bonyeza kulia kwenye ’mipaka’ na namba za chaguzi zitaonekena. Chagua ‘properties’ kutoka kwenye orodha ya chaguzi.

  Chagua ‘Style’ kwa ‘Boundaries’ layer

 3. Window itaonekana na kuleta namba za mitindo utakazochagua humo. Tutatutumia mtindo uliokwisha weka, angalia ‘Buguruni’ imeonyeshwa. Bonyeza ‘Apply’, na halafu ‘OK’ na mitindo itawekwa. Unaweza kutengeneza kanuni na mitindo mipya kwa kata nyingine kama unajua osm-id ya mpaka wake, hii inapatikana kwa kutafuta kwenye OSM.

  Buguruni, kata iliyochaguliwa, na mtindo uliochaguliwa kuwekwa

 4. Utarudishwa kwenye map canvas, ikionyesha wazi muonekano wa Buguruni. Hatua inayofuata ni kuandaa ramani kwa kuileta na kama inahitajika kuchapishwa.

  Kuchagua ‘Selecting composer’ kuandaa ramani ili kuitoa

 5. Mradi uliopakuliwa kutoka GiTHub ukijumuisha idadi ya ‘composers’, kwa huu mfano chagua ‘Buguruni-General’ kutoka kwenye orodha ya chaguzi.

  ‘Buguruni-General’ kiolezo kutoka ‘Print Composers’ menu

 6. Window mpya itaonekana  na ramani ya Buguruni ikionekana kwenye kipande cha ramani. Hiki kipande kitajumuisha vitu kama kichwa cha ramani; ufunguo; na taarifa kuhusu Ramani Huria. Kisanduku kwa upande wa kulia kwenye kioo italeta orodha ya namba ya ‘vitu’ ambavyo vinaweza kuzimwa, kuviondoa kwenye ramani ambayo itahamishwa. Unapotengeneza ramani tunapendekeza uhakikishe ramani yako ni ya kiwango cha juu kwa kuwa na kichwa sahihi, ufunguo na sifa zinazohusika.New Window
 7. Tumia vifaa kwenye sehemu ya orodha upande wa kushoto wa kioo cha compyuta(screen) kuhamisha ramani na kuweka katikati sehemu zilizochaguliwa kama inavyoitajika.

  Peleka kama PDF kutengeneza ramani katika njia inayowezwa kusomwa ambayo pia iko tayari kuchapishwa

 8. Pindi ramani inapotokea kama ilivyolengwa, uko tayari kuihamisha(exporting). Unaweza kuiweka kama picha, PDF au faili la SVG- tunapendekeza PDF kwa maana hii itafanya kua tayari kuchapishwa inapohitajika. Chagua ‘Composer’ kutoka kwenye sehemu ya orodha(menu bar) na ilete kama PDF (export as PDF) kutoka kwenye orodha ya “drop down’.
 9. Window itaonekana ikikutaka kuchagu mahali ambapo ungependa kutunza ramani na jina la faili.

Hongera, sasa umetengeneza ramani kwenye QGIS

Jifunze zaidi

Kama bado una maswali, au unahitaji msaada, timu ya Ramani Huria inafurahi kukusaidia. Fuatilia au hudhuria kwenye tukio la Maptime Tanzania na tunaweza kukupa ushauri na majibu.