drone group photo

Tarehe 7 na 8 mwezi Novemba ilikua ni mwanzo wa enzi mpya ya Ramani Huria – mradi ambao kwa kipindi cha mwaka uliopita ulileta pamoja muunganiko wa aina mbalimbali ya washirika ikiwa pamoja na Tume ya taifa ya sayansi na teknolojia, Benki ya dunia, chama cha msalaba mwekundu cha Tanzania, Marekani na Denmark,Humantarian OpenstreetMap Team, serikali ya tanzania na wanafunzi wa chuo kikuu ardhi na cha Dar es salaam kutambua uwezo wa data zilizotengenezwa kwa ramani jamii na kuendesha uvumbuzi katika mbinu za kisasa za ramani.

Watengeneza ramani za jamii, maofisa wa serikali na wataalamu kutoka sehemu mbalimbali( wa ndani na kimataifa) walipanga mstari pamoja katika meza ya usajili, tayari kwa kujihusisha na majadiliano juu ya maendeleo na uwezo wa mbinu za ramani jamii  Dar es salaam katika Makumbusho ya Taifa na nyumba ya kiutamaduni katika moyo wa Dar es salaam.

img_97811Mheshimiwa Theresia Mmbando, Katibu tawala mkoa

Asubuhi ya siku ya kwanza ilisherehekewa na wanajamii wote waliojitolea muda wao na maarifa yao yasiyolinganishwa ya Dar es salaam kutengeneza ramani zenye taarifa za kina za Ramani Huria. Hizi ramani kwa sasa zishaunganishwa katika mfumo wa atlasi kwa ajili ya kuzuia mafuriko – zimepokelewa na wajumbe wote wa mkutano wakati wakiwasili. Mheshimiwa Theresia Mmbando, Katibu tawala mkoa, na Osiligi Losai, Afisa mtendaji wa kata ya Kigogo, walitoa hotuba zao, walipongeza timu ya wanajumuiya wote wa Ramani Huria katika mafanikio yao waliyofikia na rasmi wakafungua warsha.

img_9938

Warsha kwa kiasi kikubwa ilichukua fomu nne za jopo ambazo zilikua na mada za Mafuriko Dar es salaam, Kujifunza kutoka Ramani Huria, Ramani za Mazingira ya Mjini na kuendeleza Ramani Huria. Ndani ya hizi paneli, Maafisa watendaji wa kata waliongelea kuhusu ushiriki wa mchakato wa ramani na kwa jinsi walivyozitumia ramani kuboresha usimamizi wa kata zao. Wasimamizi wa Majanga walitoa maoni katika ubora wa data zilizotengenezwa kwa ramani jamii, wataalamu kutoka mashirika ya kimataifa walitoa ushauri na msaada kwa ajili ya kuendeleza, na wawakilishi kutoka vyombo vya juu vya utoaji maamuzi walitangaza mazingatio yao ya kupitisha ramani jamii kama zoezi la kawaida na rasmi kuchanganya data za Ramani Huria katika mipango ya maendeleo.

RH CafeMgahawa wa Ramani Huria

Waliohudhuria mkutano walianzisha mjadala wa kusisimua wa maada zote zilizojadiliwa. Mjadala huu ulifanyika wakati wa mgahawa ya Ramani Huria, wakati wa kipekee ulioruhusu wazungumzaji kubadilishana utaalamu wao kwa kina na wajumbe wenye nia wakati wa kahawa na vitafunwa. Wakati mwingine uliingizwa katika tukio la mchezo wa kifedha uliohusu utabiri, ulioongozwa na Julie Arrighi wa chama msalaba mwekundu cha Marekani. Huu mchezo ulitambulisha dhana ya ufadhili inayohusu utabiri – mfumo unaotumia sayansi ya hali ya hewa na tabia ya nchi kutabiri madhara yanayowezekana katika maeneo ya hatari na kukusanya rasilimali kabla ya tukio – kupitia shughuli shirikishi iliwezekana kwa wote.

img_0110Meya wa jiji, Isaya Mwita

Kwa baraka za maofisa wakubwa wa serikali ambao walionyesha uwepo wao katika warsha, kutoka kwa katibu tawala hadi kwa meya wa Dar es salaam Mh. Isaya Charles Mwita, Timu ya Ramani Huria sasa imepewa kazi ya kuunda mipango yake mipya ya kuendeleza mradi na washirika wake – ambapo itapanuka kijiografia kwa ilipofikia na kupanua mtazamo wake zaidi ya kuzuia mafuriko. Mradi utaendelea kukuza ushirika wake – wa ndani na kimataifa – ili kuhakikisha kwamba thamani ya ushirikishwaji jamii unaenea ndani ya maeneo ya mipango miji na maendeleo, kwamba Tanzania iongoze dunia katika mbinu za ubunifu wa ramani.

Maonyesho, picha, na rasilimali nyingine zitapatikana hivi karibuni hapa: ramanihuria.org.

 

This article has 1 comments