QGIS ni chanzo huria na jukwaa la mfumo wa taarifa za jiografia (GIS). pragramu imeundwa na watu wa kujitolea kutoka kwa programu ya jamii huru na vyanzo huria (FOSS) na ipo vizuri katika msitari na mbinu ya Ramani Huria ya kutumia vifaa vya vyanzo vya wazi wakati wowote iwezekanavyo. QGIS inaendesha programu kama Linux, Unix, Mac OSX, Windows na Androids na inasaidia vector, raster mbalimbali na muundo wa database na jinsi unavyofanya kazi. QGIS pia inasaidia idadi ya programu saidizi ambazo zinaweza kutoa  kwa mtumiaji visaidizi vingi vya ziada. Moja ya hizi programu saidizi ni InaSAFE

QGIS Interface

QGIS Interface

InaSAFE ni programu saidizi kwa ajili ya QGIS ambayo inatoa picha halisi ya madhara ya maafa ya asili kwa ajili ya mipango bora, kujiandaa na jinsi ya kuchukua hatua baada ya janga. Programu imeengenezwa kwa pamoja na Indosia (BNPB), Australia (serikali ya Australia) na Benki ya Dunia (GFDRR), na inatumika dunia nzima kwa ajili ya kupanga maafa. Moja ya malengo ya Ramani Huria ni kwa ajili ya data ambayo tunaikusanya ili kutumika katika kuboresha maeneo ya mafuriko na InaSAFE inasaidia kufanikiwa katika hili kwa kuruhusu kata za Dar es salaam kuwa na ufahamu zaidi katika athari za mafuriko, hatimaye kuwezesha ufanisi ziadi wa mipango ya maafa.

InaSAFE inasaidia kuboresha utayari wa maafa kwa kutoa njia mpya za kuunganisha taarifa ya kisayansi ya maafa na maarifa ya jamii katika athari za maafa. Maafa kama tetemeko, sunami, mafuriko na volkano , pamoja na kuzingatia ufahamu wa watu, majengo na barabara zinachanganuliwa kwa InaSAFE ili kutengeneza athari halisi na ramani ya hatua kwa ajili ya mipango bora, utayari na mwitikio.

Mpangilio wa InaSAFE unaotengenezwa na Ramani Huria unalenga katika ufahamu wa taarifa za maafa ya mafuriko zinazotolewa moja kwa moja kwa idadi ya watu wa kata. Hapa chini ni muhtasari mfupi wa huu mchakato.

Hatua za kutengeneza ramani za InaSAFE

 • Ardhi oevu – tunatumia hizi kuonyesha maeneo yapi yako hatarini kwa mafuriko
 • Worldpop 25 – hii ni raster ya idadi ya watu inayochukuliwa kutoka WorldPop na inapangwa katika mita 25. Na pia tunapanga pixel za athari ipasavyo.

Jambo la kwanza sisi kufanya ni kuongeza safu katika safu ya ardhi oevu ili kuonyesha wapi ni hatari kwa mafuriko. Kufanya hivi, tunahitaji kutumia ‘field calculator’ kinachofanya kazi ndani ya QGIS. Fuata hatua hizi:

 1. Chagua safu ya wetland katika sehemu ya safu na hakikisha imeonekan
 2. Bonyeza katika safu ya kitufe katika toolbar, au bonyeza Layer -> fungua Attribute table
 3. Bonyeza katika kitufe cha ‘Editing’ katika safu ya toolbar
 4. Bonyeza katika kitufe cha ‘Field Calculator’ katika safu ya toolbar na utumie chaguzi zifuatazo kama zilivyoonyeshwa katika picha hapa chini:
  • Weka alama ya vema katika ‘Create new field’
  • Tengeneza ‘Output field name’ katika ‘FLOODPRONE’ (hakikisha unaweka katika  herufi kubwa na sahihi kama zinavyoonekana)
  • Tengeneza ‘Output field type’ katika ‘Text (string)’
  • Katika expression box ingiza ‘YES’ (kwa hili zoezi tutakuwa tumeweka kata zote kama ni hatarishi kwa mafuriko kwa kuanza nazo)

 

 1.   Bonyeza ‘OK’ katika field calculator kuthibitisha mabadiliko
 2.   Bonyeza katika kitufe cha ‘Editing’ katika safu ya toolbar
 3.   Bonyeza kitufe cha ‘Save’ ili kuhifadhi mabadiliko yako

Safu yetu Ardhi oevu sasa ina safu nyingine ya ziada inayoonyesha kwamba eneo ni hatari kwa mafuriko. Sasa tutajaribu kubadili hii ardhi oevu katika ‘NO’ kwa hali yake ya hatari kwa mafuriko ili kuona kivipi matokeo ya uchanganuzi yanaweza kuwa.

Pia, tunaenda katika safu ya ‘register’ katika InaSAFE kwa kuonyesha maneno yake makuu. Kufanya hivi, tutatumia keywords wizard. Fuata hatua kama zinavyoonyeshwa katika mfurulizo wa picha hapa chini ili kusajili safu kama ni safu ya maafa ya mafuriko.

Chagua safu ya ‘Wetland’ katika seheme ya safu na hakikisha imeonekana (inaweza kuwa tayari ishaonekana ambapo ni vizuri)

Bonyeza katika ‘InaSAFE keywords Wizard’ katika InaSAFE toolbar.

Katika hatua zinazofuata, zinaonyesha kwamba safu ni ya hatari, mafuriko, oevu / kavu na tabia ya FLOODPRONE kuwa tabia inayoonyesha kama eneo ni hatari kwa mafuriko.

Katika ukurasa unaofuata, tutaonyesha kwamba maeneo ya FLOODPRONE ni yale yenye yaliyowekwa ‘YES’. Hii imefanyika tayari kwa ajili yako kwa makusudi, hakuna haja ya kufanya chochote kwaiyo unaweza  bonyeza ‘Next’.

Baada ya kuchagua “hazard”, bonyeza ‘Next’ kuchagua aina ya safu ya hazard iliyoonyeshwa ambayo katika hali hii inatakiwa iwe “flood” kama inavyoonekana  chini.

Mara tu baada ya kuchagua “flood”, ukurasa utatokea wa kuingiza data. Chagua “wet / dry”.

Baada ya hivyo, Bonyeza “FLOODPRONE” kuchagua attribute katika safu inayoonyesha ukubwa wa mafuriko.

Tunatumia mfumo wa taifa wa orodha ya takwimu (National Bureau of Statistics-NBS), kwaiyo tutaweka chanzo  ni ‘NBS’ na tovuti ya ‘http://nbs.go.tz’. Kila kitu katika ukurasa huu ni chaguzi, kwaiyo weka taarifa bora inayopatikana. Bonyeza ‘Next’ ukiwa umemaliza.

Ongeza chanzo na tovuti ya chanzo cha data unayotumia.

Katika ukurasa wa mwisho wa Keyword Wizard, unaweza kuingiza kichwa kizuri kwa ajili ya safu. Hii itatumika katika Legend na katika ripoti. Kwa sasa tuiite ni ‘Flood prone areas’

kwa kubonyeza ‘Finish’ utakua umemaliza mchakato wa kutengeneza keyword. Sasa unaweza kuona keyword yako katika sehemu ya InaSAFE.

Kuweka kiasi cha uchambuzi

Tunakaribia kufanya uchambuzi. Kabla ya kufanya hivyo, tunahitaji kujua ni eneo gani linaweza kutumika kwa uchambuzi. Bonyeza katika kitufe cha ‘Extent Selector’

Tumia ukurasa utaotokea, bonyeza ‘select on map’ na chora kuzunguka eneo la picha.

Mwisho, bonyeza OK.

Kufanya uchambuzi

Katika hatua hii, kizimba cha InaSAFE inabidi kionyeshe kwamba uko kufanya uchambuzi wa mafuriko katika idadi ya watu. Bonyeza kitufe cha ‘Run’ kuanza mchakato wa uchambuzi. Kama kila kitu kiliwekwa sahihi, unatakiwa upate matokeo katika kizimba baada ya sekunde chache na safu mpya ya ramani inabidi iongezwe katika ramani.

Kumbuka: matokeo ya safu yanaweza kuficha safu nyingine zote – buruta safu chini ili uweze kuona mipaka ya kata juu yake. Sasa bonyeza kitufe cha ‘Print’ katika kizimba na bila kubadili chaguzi zozote, bonyeza ‘Open PDF’ katika sehemu ya matokeo ya ‘print’

Kuweka QGIS na InaSAFE

Kuweka QGIS na InaSAFE ni haraka na mchakato rahisi. Zote ni bure kutumia na zinaweza kuwekwa katika mfumo wowote wa uendeshaji. Kumbuka kwamba ili kutumia program saidizi ya InaSAFE, lazima kwanza uweke QGIS

 1. Ingiza QGIS kutoka kwenye ukurasa uliopakuliwa kwa kuchagua chaguzi sahihi kwa mfumo wako wa uendeshaji (download page by selecting the correct option for your operating system.)
 2. Pale ikishaingizwa (ipakue kutoka  http://download.qgis.org), fungua programu
 3. Kutoka kwenye menu kuu, nenda kwenye Plugins > Fetch Python Plugins na utafute InaSAFE. Ichague na ubonyeze kitufe cha ‘Install’. InaSAFE sasa itakuwa imeongezeka katika menyu ya program saidizi. Tunakuhamasisha utumie toleo la ‘LTR’ la QGIS (wakati wa kuandika 2.8.2) kwani hili litakua ni toleo bora na tutahakikisha kwamba InaSAFE inafanya kazi na toleo la LTR la QGIS.
 4. Program saidizi ya InaSAFE ni mara kwa mara huendelezwa na pia inawezekana kuweka toleo la kisasa la majaribio, kwa mengi Zaidi angalia kwenye InaSAFE installation guidance.

Kutumia QGIS na InaSAFE pamoja na OpenStreetMap

Unaweza kutumia data za OpenStreetMap katika QGIS, ambapo ni bora kwa Ramani Huria kama hii ndio kiini cha kazi zetu za ramani. Safu katika QGIS zinaweza kuhifadhiwa kama shapefiles, executive filters, queries na kadhalika.

Kuna njia mbalimbali za kupata data za OSM katika QGIS. Unaweza kuomba data katika server ya OSM, sawa na jinsi ungweza katika JOSM, lakini tunakushauri matumizi ya built-in download function katika QGIS, ambayo inaweza kupatikana kwa kwenda : Vector -> OpenStreetMap -> Download Data. Kwa hatua kwa hatua elekeza kuingiza data za OSM na kutengeneza safu, see the section on QGIS on learnosm.org.

Tovuti ya InaSAFE (The InaSAFE website also provides a largest amount of data that can be downloaded) pia inatoa kiasi kikubwa cha data ambazo zinaweza kupakuliwa ili kukusaidia wewe kujifunza Zaidi kuhusu program saidizi na matokeo ya mazoezi kwa data za sampuli. Kwa kutumia mfano huu ni njia kubwa ya kupata taarifa za InaSAFE.

QGIS na InaSAFE katika mazoezi ndani ya Dar es salaam

Ramani Huria inatumia OpenStreetMap kuunda ramani za kisasa na sahihi za baadhi ya kata kubwa ambazo ni hatarishi kwa mafuriko za Dar es salaam. Ramani hizi zinaweza kutumika kama msingi wa uchambuzi katika InaSAFE na andaa matokeo halisi ya maafa ya asili kwa mipango bora na mwitikio kwa kulingana na mahitaji ya jiji. Ukurasa wetu wa GitHub unahusisha mradi wa QGIS kama unamilikiwa na Ramani Huria kutengeneza ramani za kuonyesha mifereji ya maji na kwa ujumla. Muundo wa ramani umelenga katika muonekano wa OpenStreetMap, lakini imechukuliwa kuonyesha taarifa Zaidi katika mitaro, mtandao wa maji, aina za majengo na matumizi ya ardhi, miongoni mwa taarifa nyingine. Zaidi ya hayo Ramani Huria inataraji kufanya kazi na ofisi ya waziri mkuu ya Tanzania, idara ya maafa katika kutafuta uwezekano wa kutumia data zilizoandaliwa wakati wa mradi huu kwa uwezo wake mkubwa.

Jifunze zaidi

Ramani Huria imefanya warsha ya siku mbili ya InaSAFE Dar es salaam kwa nyenzo za kufundishia ambazo zinapatikana GitHub, bure kupata na kutumia. Nyenzo pia zinatoa mfano halisi wa somo la mafuriko ndani ya Dar es salaam ili uweze kuona jinsi QGIS na InaSAFE inavyotumika kwa vitendo kwa mahitaji ya Tanzania.

Kama zote QGIS na InaSAFE zilivyoundwa kwa program za jamii huru na za vyanzo vya wazi, wana jamii za mtandaoni na nyenzo nyingi za bure za mafunzo zinapatikana. Hizi ni sehemu mbalimbali za kujifunza zaid:

 • Maelezo kwa mtumiaji wa QGIS (The QGIS user guide) yanakupa maelekezo ya taarifa zote za QGIS.
 • Nyenzo za kufundishia QGIS (The QGIS training manual) ni maelezo ya mafunzo ambayo yanaelekeza wasomaji katika vitendo vyote watakayotaka kufanya ndani ya program.
 • Nyaraka ya InaSAFE (InaSAFE documentation) inatoa maelezo ya vitu vyote vya InaSAFE
 • Ukurasa wa nyenzo za mafunzo ya InaSAFE (The InaSAFE training materials page) una utajiri wa nyenzo zinazotoa hatua kwa hatua mafunzo katika kutumia OpenStreetMap na InaSAFE pamoja na QGIS

Kama utakuwa na maswali au unahitaji msaada, timu ya Ramani Huria inayo furaha kukupa msaada! Tufuatilie (Get in touch) au njo katika matukio ya Maptime Tanzania ambapo tunakupa ushauri wowote unaouhitaji.