Katika kazi ya Ramani Huria ya utafiti wa ramani, wanajamii wamekuwa ni sehemu ya mchakato. Uwepo wao umeleta mafanikio makubwa na kuwahi kumalizika kwa uandaaji ramani katika kata zao.

Kwa nini tunatumia wanajamii?

  • Wanauelewa wa ndani kuhusu eneo lao wanaloishi. Hii inamaanisha, wanajua ndani na nje ya maeneo yanayoandaliwa ramani kutokana na ukweli kwamba wamezaliwa pale au wameishi hapo kwa muda mrefu. Kiuhalisia, wanajamii wameweza kuwaongoza timu ya Ramani Huria kwenye maeneo hatarishi na maeneo mengine muhimu kwa msaada wa picha za anga.
  • Wanehakikisha usalama kwa waandaaji ramani(wanafunzi wa Chuo Kikuu), kutumia uanajamii wao kudhamini uwepo wa waandaaji ramani ndani ya jamii. Hii inafanya urahisi kwa waandaaji wa ramani kukusanya taarifa na kutengeneza ramani katika kata ambazo wakazi wanaoweza kuleta vurugu au wanakataza vitu vyao visiwekwe kwenye ramani kutokana na hofu ya kuuzwa ardhi au nyumba zao. Kwahiyo, wanakua sehemu ya jamii ya OSM na kupitia hii, wanafundishwa njia za kutengeneza ramani kama jinsi ya kutumia GPS, OSM trackers, JOSM n.k. Kwa matokeo, wanajamii wanafundishwa kisawasawa ili waweze kuwa wanaingiza taarifa mpya hata kama mradi wa Ramani Huria ukiwa umeisha katika kata yao.

Hatua:

  • Kama hatua ya kwanza, mipango ya kuandaa ramani inafanywa kupitia Afisa Mtendaji wa Kata. Hii ni muhimu kwa uhalali wa mradi kwa kuwa utengenezaji wa ramani unatakiwa upitishwe na kuhararishwa na Afisa Mtendaji wa Kata. Kwa kuongezea, Afisa Mtendaji wa Kata anaweza kupendekeza viongozi wa wanajamii wawajibikaji na wanachama wa mitaa inayounda kata husika.
  • Baada ya hapa, siku ya kufungua kikao cha wanajamii inapangwa kutambulisha shughuli za kuandaa ramani. Washiriki wanaoalikwa ni wanajamii, waandaaji ramani, Afisa Mtendaji wa Kata na jopo la viongozi wa mitaa, na vilevile timu ya Benki ya dunia/Humanitarian OpenStreetMap. Kikao kinaanza na utambulisho wa malengo ya mradi na kufuatiwa na mafunzo ya jinsi ya kutumia kifaa cha GPS, OSM trackers, JOSM n.k. Katika hiki kikao, wanajamii wanajadili kuhusu maeneo ambayo yanaathiriwa na mafuriko kwa sana katika kipindi cha mvua.
  • Hatua inayofuata ni kuanza shughuli za kuandaa ramani kwa msaada kutoka kwa wanajamii na waandaji ramani. Mara wanapofunzwa kutumia karatazi za picha ya satelaiti zinazotengenezwa kwa kutumia picha za ndege isiyokuwa na rubani(drone), muandaaji ramani, anasindikizwa na mwanajamii mmoja kuelekea mahali pa kuchukua/kuhakiki taarifa. Wanapoenda kuchukua taarifa, muandaaji ramani na mwanajamii wanafuata muundo wa taarifa wa Ramani Huria kuchukua taarifa za majengo, barabara, maeneo hatarishi, mitaro, maeneo muhimu n.k. Wanajamii wanashiriki zaidi kwa kuchangia mawazo yao kwenye mitaa wanamoishi. Taarifa zote zinachukuliwa kwenye fomu za kujazia taarifa vilevile katika kifaa cha GPS au OSM tracker.

Muandaaji ramani na mwanajamii wakikusanya taarifa.

  • Baada ya ukusanywaji wa taarifa, waandaaji ramani na wanajamii wanarudi mahali pakukutania na jopo zima la Ramani Huria. Mahali pa kukutania mara nyingi zinakuwa ofisi za kata au shule za misingi, inategemea na upatikanaji wa nafasi ya kufanyia kazi inayoruhusu kazi za kuandaa ramani kufanyika.
  • Kipindi waandaaji ramani na wanajamii wanapofika mahali pa kukutania, zoezi la kuingiza taarifa linaanza. Hii inafahamika kama kudijitaizi, ambapo waandaaji ramani na wanajamii wanatumia JOSM kuhamisha taarifa zilizokusanywa kwenda kwenye mfumo wa taarifa za OSM. Hii inakuwa kazi ya kila siku ambayo inafanywa mpaka kata nzima ikamilike.

Muandaaji ramani na mwanajamii wakiwa katika kipindi cha dijitaizesheni.

  • Kipindi cha uandaaji ramani, ukaguzi wa kila siku wa taarifa unafanyika na wasimamizi wa kata. Hii inafanyika kuhakikisha taarifa zinazodijitiziwa zinakuwa na kiwango kizuri na kosa lolote linarekebishwa. Kwa mara nyingi, mitaro hupewa umakini mkubwa kwa sababu ya uhitaji wa muunganiko wake. Baada ya Mitaro, majengo, sehemu za huduma na barabara zinapewa kipaumbele. Kama kuna taarifa yenye kasoro au inahitajika kuhakiki kwenye eneo husika, timu nyingine ya waandaaji ramani na wanajamii inatumwa kuhakiki taarifa ya eneo husika.

Wanajamii wawili na muandaaji ramani mmoja wakati wa uhakiki wa taarifa.

  • Baada ya kusafisha taarifa, hatua ya muhimu inayofuata ambayo ni, kutengeneza ramani za kata. Ili kuweza kutengeneza hizi ramani, shapefiles zinachotwa kutoka tovuti ya HOT export tool. Waandaaji ramani na wasimamizi wanahusika na utengenezaji wa hizi ramani kwa kutumia QGIS. Katika utengenezaji ramani, wanajamii wanaovutiwa wanafundishwa jinsi ya kutumia QGIS na jinsi ya kuchambua eneolao. Ramani Huria pia inatoa nakala zilizochapwa za ramani ya kata kwa ujumla na ramani ya mitaro kwa Afisa Mtendaji wa Kata ili kuwezesha mipango ya majanga, kuzuia na mwitikio ambao utasaidia kupunguza uhalibifu na upotevu.
  • Pindi ramani zimeshatengenezwa, tarehe ya kufunga kikao zinapangwa na wanajamii wanapewa taarifa na viongozi wao. Katika mkutano, ramani zilizotengenezwa zinakabidhiwa rasmi kwa Afisa Mtendaji wa Kata na wanajamii wanaohusishwa kwenye mradi wanapewa vyeti vya ushiriki.

Msimamizi wa uandaaji ramani akiwa (amevalia tisheti nyeupe) akikabidhi ramani kwa afisa mtendaji na wanajamii wake katika kikao cha kufunga mradi kata ya Vingunguti.