Tandale ni kata iliyoko magharibi mwa wilaya ya Kinondoni iliyo na makazi mengi yasiyo pangwa. Inakadiriwa kuwa na takriban watu 54,781. Tandale imegawanya na mkondo wa Kwamkunduge na ina eneo kubwa la mafuriko. Baadhi ya nyumba zimeachwa kwa ajili ya mafuriko.

Eneo hili lilichorwa kwenye ramani huria mnamo mwaka 2011. ramani hii iliboreshwa mwezi wa aprili hadi may mwaka 2015 kwa kutumia picha za ndege ndogo iitwayo “drone” zilizochukuliwa na timu yetu.