Ndugumbi ni kata ndani ya wilaya ya Kinondoni iliyopo upande wa magharibi wa Dar es Salaam, yenye wakazi takribani 36,841 kutokana na taarifa za sensa ya mwaka 2012. Ndugumbi ina baadhi ya maeneo yaliyopagwa ila pia ina maeneo mengi yasiyo na mpangilio. Pia kata hii ina maeneo mengi yaliyo kwenye maeneo ya mafuriko, maeneo yaliyo karibu na mkondo wa Kwamtunduge.

Ramani ya kata hii, ilichorwa na wanachama wa Dar ramani huria kwa takriban siku 30, wakiwa na wanajamii 10 na wanafunzi 15 wa chuo kikuuu cha ARDHI ambao walikuwa wanahamu yakuchangia ukusanyaji wa taarifa na kuchora ramani.