p>Warsha ya mafunzo ilifanyika tarehe 26, March pale Buni Innovation Hub, kwenye kamisheni ya sayansi na teknolojia.

Jopo: Uvumbuzi wa mafuriko mijini

Kutatua changamoto za mafuriko mijini – Uvumbuzi na fursa.

Rekha Menon, Kiongozi wa mradi, Benki ya Dunia.

Prof. Robert Kiunsi, Mkuu wa shule ya masomo ya Real Estate (SRES), Chuo Kikuu Ardhi.

Juliana Letara , mkuu wa idara ya mipango miji manispaa ya Kinondoni.

Dr. Bob Day, Mkurugenzi wa Non-Zero-Sum Development.

Jopo la kwanza lilianza miendelezo kwa mahojiano ya juu katika kupambana na hatari ya mafuriko mjini Dar es Salaam na fursa za kuungana na taasisi zingine Dar es Salaam. Mgeni rasmi Patrick Makungu, Katibu Mkuu wa wizara ya sayansi, mawasiliano na teknolojia ambae alionesha uhitaji wa kupambana na mafuriko mijini na umuhimu wa kuwekeza kwenye sayansi na teknolojia kwa ajili ya kukuza uvumbuzi kwenye suala hili. Hili lilipazwa sauti na wasomi kuwa ili ramani za jamii ziwe endelevu, ujengaji wa ujuzi kwenye taasisi za serikali na wasomi lazima zitokee; na ujengaji wa mitaala kwenye kuchora ramani. Kutoka kwenye pointi hii tutahitaji data sahihi kwenye kiwango cha jamii ili kubaini hatari ya mafuriko na athari kwa wananchi.

Jopo: Kuchora ramani kupambana na mafuriko

OpenStreetMap–Kuweka sauti ya jamii kwenye mfumo wa digitali

Red Cross– Onyo la mwanzo na tendo la mwanzo

Osiligi Lossai, Afisa mtendaji wa kata, Tandale

Prof. Herbert Hambati, Profesa wa Jografia, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Charles Msangi, Disaster Focal Point, Idara ya menejimenti ya maafa.

Dr. Vedast Makota, Mkurugenzi wa muda, taarifa mawasiliano ya mazingira na kufikia.

Julie Arrighi, Mshauri wa mapambano Africa, American Red Cross

Jopo la pili lilielezea kwa upande wa kiufundi wa kuchora ramani za jamii na uhitaji kwa angalizo/onyo la kwanza la mafuriko, na maongezi kutoka timu ya Humanitarian OpenstreetMap na Red Cross. Hii ilifungua mjadala wa jopo na wataalam wa kiufundi kutoka serikalini na wasomi kuhusu mbinu na utumiaji wa data kutoka kwenye miradi inayoendelea ya kuchora ramani mpaka kwenye maswali. Hizi zilihusu maswali maalum kama vile data zitakwenda wapi na nani atakuwa na wajibu kwa kujaribu ubora na utunzi. www.openstreetmap.org itakuwa inaweka data pale zinapokuwa zimetengenezwa, na tunakaribisha wachangiaji wa data kuchunguza, kushiriki na kujaribu data.

Jopo: kushirikisha jamii

mwanzo/maandalizi : kushirikisha jamii

mwanzo/maandalizi : kushirkiana na kuwa mstari wa mbele wa maandalizi na misaada ya maafa

Dr. Tim Ndezi, mkurugenzi , kituo cha mipango ya jamii

Teemu Seppälä,mshauri wa uvumbuzi , TanzICT

Angela Ambroz,mwanasayansi mtaalamu wa taarifa za maendeleo , Twaweza

Brian Paul, meneja wa kitovu cha uvumbuzi, Buni Innovation Hub

David Mlimilwa, mjumbe wa mpango – Kenya, shirika la msalaba mwekundu Dernmark

Renatus Mkaruka, meneja misaada wa maafashirika la msalaba mwekundu Tanzania

Jopo la mwisho lilijadili umuhimu wa kushirikiana katika ngazi ya ndani na yakimataifa , wakijadili mifano ya ramani za jamii kama za Tandale na jinsi ushirikiano unavyoendelea na global maping projects ”missing maps ” (ramani zakimataifa) ambapo watu wanaojitolea wanasaidia kuchora ramani wakati wa mafuriko.ushirikiano