Sanaa ya Ramani za Mifereji ya Maji Dar es Salaam.

Moja ya malengo makubwa ya Ramani Huria 2.0 ni kuongeza juhudi zilizofanyika kwenye ramani za mifereji zilizofanyika wakati wa majaribio ya mradi. Wanafunzi sasa wamegawanywa katika makundi mbalimbali ili kurahisisha uratibu na kuwapanga kulingana na ujuzi.Makundi haya ni pamoja na; Timu ya mifereji, Timu ya GIS, Timu ya  Open map kit,Timu ya kuwafikia wana jamii,na timu ya kutengeneza ramani za mbali.(bila kuwa sehemu husika) Hakukuwa na njia inayojulikana ya kutegeneza ramani za mifereji, Hivyo timu  yetu ilibidi kujaribu njia mbalimbali zinazofahamika za kutengeneza ramani, baada ya kujaribu, Kipengele cha Geotrace pamoja na uwezo…Read more

Kudhibiti Ubora Katika Kutengeneza Ramani za Mbali

Kupanua mradi wa kutengeneza ramani kwenye mji wenye watu zaidi ya milioni tano unahitaji mipango na mafunzo sahihi. Tulipenda kwanza wanafunzi wetu wapate  maelezo ya kina ya jinsi taarifa  inaingizwa kwenye OSM ili kuhakikisha uelewa wazi wa mazingira ya OSM na jinsi inavyofanya kazi. Katika hatua ya baadaye, tutawaonyesha jinsi taarifa ya OSM inaweza kutumika kwa madhumuni kadhaa tofauti. Kufundisha wanafunzi mia tatu kutengeneza ramani, huja na changamoto kadhaa. Wanafunzi  wetu wote ndio wanaanza, na wengi wao hawajawahi kuchangia kwenye OSM kabla. Kazi yao ya kwanza ilikuwa rahisi- kufungua akaunti za OSM, kusainiwa…Read more

Utengenezaji Ramani kwa Kasi

Timu mpya na iliyoongezwa ya Ramani Huria 2.0, yenye hadi zaidi ya wanafunzi mia tatu, kwa sasa ipo katika mazoezi ya vitendo ya kukusanya taarifa na kuhariri ramani ya kidigitali ya Dar es Salaam. Tumeweka OpenDataKit (ODK), programu huru inayotumika kukusanya taarifa kwenye simu za smatifoni. Tutatumia mitandao mingine ya kisasa zaidi katika kukusanya taarifa kama vile OpenMapKit, programu ya haja ya ODK ambayo inaruhusu maingiliano ya moja kwa moja na taarifa za OpenStreetMap, lakini programu ya kuheshimika na yenye nguvu ya ODK ni nzuri kwa kuanzia. Tulianza kwa kufanya mazoezi ya vitendo…Read more

Wanafunzi Mia Tatu Kutengeneza Ramani za Kuzuia Mafuriko Dar es Salaam

Humanitarian Openstreet Team (HOT) na Ramani Huria, wakifadhiliwa na benki ya dunia na wadau wengine wameanzisha safari mpya na Chuo Kikuu Ardhi! Wanafunzi mia tatu wa Mipango Miji na Geomatics kutoka Chuo Kikuu Ardhi jijini Dar es salaam wanashiriki katika mradi wa kutengeneza ramani za jamii mwezi Julai na Agosti.Tutatengeneza ramani za kata 35 jijini,msisitizo ukiwa katika taarifa zinazohitajika ili kuzuia mafuriko. Kwa ongezeko la athari za mabadiliko ya tabia ya nchi na ukuaji wa miji, mafuriko mjini yamezidi kuvuruga na kutishia maisha ya watu wa Dar es Salaam. Ili kusaidia watu jijini,…Read more