Kutengeneza Ramani

 

Mara nyingi  au chache, ramani hutenegenezwa remotely na wasanifu wa ramani kwa uweledi mkubwa katika kazi zao, lakini hakuna uhalisia kutoka katika eneo halisi wanalo lifanyia kazi. Kwa mfano wa ramani zinazochanganya kutoka eneo moja la Dar es salaam zilizopigwa sawa sawa.

Ramani Huria hivyo hivyo inafanya kazi kwa utofauti. Tumewafunza wanafunzi kutoka chuo kikuu na wananchi jinsi ya kutengeneza ramani kwa urahisi mkubwa katika maeneo wanayoishi-ramani ambazo zinatarifa zilizokamilika kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya maendeleo.

untitled-design


Ukusanyaji Data

Dhumuni la kwanza la Ramani Huria ni kuwaanda wanajamii kwa ujuzi unaotakiwa kutengenezea ramani. Ili kufanya hivyo tunaanza na kuwaelimisha washiriki wa mradi katika njia mbili tofuti za kukusanya data:

  1. GPS na Karatasi kazi
  2. OpenMapKit na Programu za OpenDataKit

Njia ya kwanza ni njia ya kawaida ya kukusanya taarifa ambayo inahusisha utengenezaji wa karatasi kazi kwa ajili kazi, kuchukua GPS na karatasi za kuandikia data zilizokusanywa, kisha unakwenda eneo la kazi kwa ajili ya lukusanya data, wakati Njia ya pili ikihusisha kuweka programu za simu ambazo zimeandaliwa picha na fomu ya kujazia data kwa ajili ya kukusanya data moja kwa moja wakati ukiwa eneo la kazi.


Picha ya Kutoka Angani

Kabla ya Ramani Huria – picha ya kutoka angani kwa ajili ya ramani ya Dar es salaam ulikua tegemezi kwa kiasi kidogo au kutokua na mawingu, au wakati mwingine ulikua ubora wa chini wa satelaiti.

Kwa kukabiliana na hili, na kuhakikisha ubora wa hali ya juu wa picha kwa wanajamii wanaotenegeneza ramani.,tulitumia ndege ndogo zisizokua na rubani kwa kushirikiana na wataalamu wa ndege hizo pamoja na tume taifa ya sayansi na teknolojia COSTECH. Tofauti kwa undani iliyowezeshwa na vifaa hivi ni ya kushangaza, inayothibtika kwa kuhusianisha ramani iliyotengenezwa kwa na bila picha za anga.

screen-shot-2015-08-14-at-1-55-26-pmBefore

screen-shot-2015-08-14-at-1-57-22-pmAfter


Picha Halisia za Mitaa

untitled-design-1

Kwenda kiundani zaidi ili kuwasaidia watengeneza ramani kuweka taarifa zaidi  kwenye ramani za eneo husika – Ramani Huria imetengeneza picha halisia za mitaa. Kupiga picha za namna hii , kuna njia tatu zinatumika: kuweka garmin camera  katika usafiri wowote ule, kuweka programu ya simu ya kutengeneza ramani ya Trimble MX7 kwenye bajaji, na kutumia programu ya simu ya Mapillary.