Kuchora

 

Baada ya kukusanya taarifa, watengeneza ramani kutoka ramani Huria walisaidia kutengeneza ramani kwa kuchora kupitia OpenStreetMap, ni jukwaa la tovuti linalofanya kazi ya kutengeneza ramani za wazi na bure ndani ya Dunia. Ramani Huria ilifundisha zaidi ya wanajamiii 200 na wanafunzi namna ya kutumia programu kwenye kompyuta, JOSM, ambapo taarifa zinaongezwa moja kwa moja katika OSM. You can view the training material here.

Matokeo ya kujitolea kwa watengeneza ramani, zaidi ya kata 25 ndani ya Dar es Salaam, zilipitiwa na kuchorwa  kwa umakini, maafisa kutoka katika kata husika kwa sasa wanaodhi vifaa hivi hadimu kuwaongoza katika maendeleo


29108260413_bb1e829b46_oOpenStreetMap ni nini?

Openstreetmap  ni mradi wa kimatandao, uliotengenezwa kwa watu wa kujitolea ambao wanfanya survey kwa kutumia GPS, wanahariri picha ya anga na kukusanya na kuhalalisha shughuli zilizopo za uma kwa kutumia taarifa za kijografia. Kwa kutumia takwimu huru  utumiaji wa takwimu kwa wote kilabli 1.0 (commons Open Database License 1.0), watumiaji wa OSM, wanamiliki, kuboresha  na kuchangia taarifa za ramani na Umma. Kuna ramani zilizo katika hali ya  kidigitali kwenye mtandao, lakini nyinginezo nyingi zina kinga za kisheria au za kiufundi.  Hii inaleta  ugumu kwa watu, serikali,watafiti pamoja na wanataaluma, wanumbuzi na matumiaji wengine kupata na kutumia taarifa kiurahisi na kwa bila gharama. Kwa kutumia OSM vyote ramani zilizo katika mtandao na zile ambazo hazijafanyiwa kazi inawezekana kuzipakua kwa matumizi mengineyo na kwa watu wengine.

Maeneo mengi ya dunia, maalum kwa maeneo ambayo hayajaendelea  kama vile Tanzania hamna motisha kwa makampuni ya kutengeneza ramani ili kupata takwimu. Kutokana na hilo, OSM ni njia mbadala kwa maendeleo ya uchumi, msaada wa haraka, mipango miji, na matumizi mengine mengi.

Kwanini tunatumia OpenStreetMap?

Ubora data za kijiografia inaweza kusaidia mashirika, jumuiya, kama vile umma kwa ujumla na serikali katika kufanya maamuzi yanayohusu masuala mengi muhimu, kama vile mazingira, uchumi, kijamii na usimamizi wa mgogoro. Jijini Dar es Salaam na maeneo mengine mengi, Ubora wa data kama hii  imekuwa pungufu au hazipatikani. Watengenezaji wa ramani wakujitolea, kama wale wanaoshiriki katika mradi Ramani Huria, wanaweza kuchangia kwa kutoa taarifa zinazohitajika, kama vile kwa kuongeza majengo, njia za usafiri, na miundombinu mingine muhimu ili kusaidia maendeleo kwamba uwezekano inategemea habari hii.

Unaweza kuchangiatu Internet na taaluma ya  kompyuta, hata kama wewe hata kama wewe haupo kwenye eneo hilo unaloandalia ramani. Unaweza kutumia picha za anga na kuonyesha barabara, majengo, ardhi, na eneo la muhimu; unaweza pia kuongeza maelezo ya ziada kuhusu vitu ambavyo tayari viko kwenye ramani. Hii data inaweza kutumika baadaae katika matumizi mbali mbali katika maeneo yanayoendelea.

Ni jinsi gani naweza kutumia OpenStreetMap?

Unaweza kujiunga na sisi katika sherehe za Ramani huria  jijini Dar es Salaam au jionganishe na sisi katika mtandao wa kijamii kwa kubonyeza hapa

Ukotayari kuanza kuandaa ramani? Unaweza kuanza kujiaunga na akaunti kwenye openstreetmap.org.