Dar Ramani Huria ni mradi wa kijamii wa kuchora ramani jijini Dar es Salaam, Tanzania. Dar Ramani Huria inafundisha timu ya wanafunzi wa chuo kikuu na wanajamii kutoka maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam kutumia OpenStreetMap kutengeneza ramani za kisasa na zenye ubora wa hali ya juu katika maeneo 17 ya jiji. Maeneo haya ya makazi (yanayojulikana kama kata) yalichaguliwa kwa sababu yanaathiriwa na mafuriko kwa kiwango kikubwa.

Katika kipindi cha mvua kila mwaka, Dar inateseka kwa mafuriko makubwa ambayo hubomoa barabara, huvunja nyumba, na matokeo ni vifo vingi na uharibifu unaogharimu mamilioni ya dola. Uharibifu ambao hufanywa na mafuriko haya unaweza kuzuiwa kwa mipango ya kutosha, lakini maeneo mengi ya jiji yamejengwa kwa kutokuwa na mipango na makazi yasiyo rasmi. Na hapo ndipo Uchoraji ramani huja. Kwa kuwasaidia wanajamii kuchora ramani za maeneo ya makazi, barabara, mikondo ya maji, mabonde na vitu vingine muhimu, mradi utaleta mpango wa kuzuia maafa na kupunguza hatari kwa kiwango cha chini, wakati ukifundisha washiriki ujuzi wa kompyuta na kuchora ramani ili waweze kutumia sehemu zingine.

Ramani zikiisha kutengenezwa, zitajumuishwa na data zingine kwenye InaSAFE, programu huru ambayo inawawezesha watumiaji kufanya utafiti wa kweli wa mazingira ya maafa asilia kwa ajili ya kupanga na kupata majibu (muitikio). Kama nyongeza ya faida, ramani hizi zitakuwa zikipatikana kwa umma kwenye mitandao, zikipatikana kwa ajili ya kupakua kwenye tovuti hii, na pia zitawasilishwa kwenye mfumo ulioprintiwa kwa serikali ndogo za kila kata.

Dar Ramani Huria inaungwa mkono na mpango wa Benki ya Dunia wa “Global Facility for Disaster Reduction and Recovery”. Ilianzishwa mwaka 2006, “Global Facility for Disaster Reduction and Recovery” GFDRR ni ushirikiano wa nchi 39 na mashirika ya kimataifa 8 ambayo yamejipanga kusaidia nchi zinazoendelea kupunguza mazingira magumu kwa majanga asilia na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Lengo la ushiriki ni kupunguza majanga hatari (DRR) na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi (CCA) katika mikakati ya kimaendeleo ya nchi kwa kusaidia mfumo wa utekelezaji nchi wa Hyogo Framework for Action (HFA). Mkataba wa ushiriki wa GFDRR, uliorekebishwa mwezi Aprili 2010, unaweka mpango awali, mantiki, na muundo wa utawala.

Partners